Kaimu Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. John Kuchaka, akizungumza wakati akifungua warsha ya siku moja iliyokutanisha Serikali na wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, kutoka mikoa ya Kigoma, Dodoma, Kagera, Mara, Manyara,Tabora, Rukwa, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita, Tabora na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkandarasi, jijini Dodoma.

Afisa Usimamizi wa Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Omar Mkima, akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja zilizoibuliwa, katika warsha iliyoratibiwa na Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, kwa lengo la kujenga uelewa na kubadilishana uzoefu kuhusu ushirikiano wa Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, katika ukumbi wa Mkandarasi, jijini Dodoma.

Mchumi kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Elias Amede, akiwasilisha mada kuhusu Mwongozo wa Bajeti ya Serikali, katika warsha kwa mashirika yasiyo ya kiserikali iliyoandaliwa na Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkandarasi, jijini Dodoma.

Mchumi Mwandamizi Wizara ya Fedha, Bw. Hezbon Magesi, akiwasilisha mada kuhusu Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo (DCF), katika warsha iliyokutanisha washiriki wa mashirika yasiyo ya kiserikali iliyoandaliwa na Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, yaliyofanyika katika ukumbi wa Mkandarasi, jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika warsha ya siku moja iliyokutanisha wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, mikoa ya Kigoma, Dodoma, Kagera, Mara, Manyara,Tabora, Rukwa, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita, Tabora na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkandarasi, jijini Dodoma.
Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Manyara Bi. Anna Emmanuel, akichangia mada katika warsha ya siku moja iliyokutanisha wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, mikoa ya Kigoma, Dodoma, Kagera, Mara, Manyara,Tabora, Rukwa, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita, Tabora na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkandarasi, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Shirika la Doyodo Tanzania, Rajabu Juma, akichangia mada katika warsha ya siku moja iliyokutanisha wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, mikoa ya Kigoma, Dodoma, Kagera, Mara, Manyara,Tabora, Rukwa, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita, Tabora na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkandarasi, jijini Dodoma.

Mchumi kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Lusubilo Mwangunga, akiwasilisha mada kuhusu mwongozo wa uzingatiaji fedha na ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali, katika warsha ya siku moja iliyokutanisha wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, mikoa ya Kigoma, Dodoma, Kagera, Mara, Manyara,Tabora, Rukwa, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita, Tabora na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkandarasi, jijini Dodoma.

Kaimu Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. John Kuchaka (katikati), akiwa katika picha ya pamoja washiriki baada ya kuhitimisha warsha ya siku moja iliyokutanisha wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Bara, kutoka mikoa ya Kigoma, Dodoma, Kagera, Mara, Manyara,Tabora, Rukwa, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita, Tabora na Arusha, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkandarasi, jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
…………………
Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma.
Wizara ya Fedha imebainisha kuwa itaendelea kujenga uelewa, kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini ili kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kijamii unakuwa na ufanisi mkubwa.
Hayo yalibainishwa na Kaimu Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. John Kuchaka, wakati akifungua warsha iliyowakutanisha Serikali na wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkandarasi, jijini Dodoma.
Alisema jitihada za Serikali ya Tanzania zimekuwa zikilenga kuhakikisha kuwa maendeleo ya wananchi yanapatikana kwa njia jumuishi na endelevu ambapo mchango wa mashirika hayo ni muhimu katika kufikisha huduma kwa jamii na kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye sekta mbalimbali.
‘‘Kupitia warsha hii mafunzo yatatolewa kuhusu masuala muhimu ikiwemo mwongozo wa kufuata taratibu za kifedha kwa wadau wasio wa kiserikali, mwongozo wa bajeti ya Serikali pamoja na miongozo ya uratibu na ushirikiano wa maendeleo ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mifumo na taratibu zinazosimamia shughuli hizo,’’alifafanua Bw. Kuchaka.
Aliongeza kuwa kupitia mafunzo hayo Serikali inatarajia kujenga uwezo wa wadau wote katika kuhakikisha kuwa shughuli za mashirika zinaendana na vipaumbele vya taifa huku zikifuata taratibu zilizowekwa kwa ajili ya kuleta matokeo chanya kwa wananchi.
Bw. Kuchaka alitoa rai kwa washiriki hao kutumia fursa hiyo kubadilishana uzoefu na kubaini maeneo ya kuboresha ushirikiano huku msisitizo ukiwekwa katika kuongeza uwazi uwajibikaji na ufanisi katika utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo nchini.
Nao baadhi ya washiriki wa warsha hayo, akiwemo Mkurugenzi wa Shirika la Doyodo Tanzania, Rajabu Juma pamoja na Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Manyara Bi. Anna Emmanuel, wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuimarisha mazingira ya ushirikiano na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ili jamii iendelee kunufaika na huduma zinazotolewa na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Warsha hiyo ya siku moja iliwakutanisha wadau kutoka Serikalini na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka mikoa ya Kigoma, Dodoma, Kagera, Mara, Manyara,Tabora, Rukwa, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita, Tabora na Arusha.
