Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Habib African, Bw. Faraz Haider (Kushoto) na Mwenyekiti wake wa Bodi wa Benki hiyo anayemaliza muda wake, Bw. Zain Habib (kulia), baada ya kikao chao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaaam, ambapo wamezungumza fursa mbalimbali zilizopo nchini hasa katika uwekezaji katika Nyumba za makazi za bei rahisi katika miji inayokuwa kwa kasi nchini.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kulia) Akimkabidhi zawadi ya baadhi ya bidhaa za kilimo zinazozalishwa nchini, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Habib African, Bw. Faraz Haider, baada ya kikao chao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaaam, ambapo wamezungumza fursa mbalimbali zilizopo nchini hasa katika uwekezaji katika Nyumba za makazi za bei rahisi katika miji inayokuwa kwa kasi nchini. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WF, Dar es Salaam)
