Na. Meleka Kulwa- Fullshangwe Blog, Bungeni Dodoma 

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Wizara ya Maji ya Sh trilioni 1.12 kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuendelea kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama nchini.

Bajeti hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), inalenga kutekeleza miradi mbalimbali ya maji mijini na vijijini, kuongeza upatikanaji wa maji pamoja na kuimarisha miundombinu ya huduma hiyo muhimu kwa wananchi.

Kupitishwa kwa bajeti hiyo kunatarajiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji na kusaidia kufikia malengo ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata huduma ya maji nchini.