Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiweka Saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri, wakati alipowasili Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma kushiriki Ibada ya Mazishi ya Askofu Shauri, leo tarehe 06 Mei 2026. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma kushiriki Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Marehemu Askofu Stanford Shauri, Ibada inayofanyika Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma leo tarehe 06 Mei 2026.