Na John Bukuku – Dar es Salaam
Kituo cha NuLife Advanced Fertility Centre kinaendelea kujijengea sifa kama mtoa huduma kinara wa tiba za uzazi nchini Tanzania, kikitoa huduma za kisasa zinazolenga kuwasaidia wanandoa wenye changamoto za kupata watoto.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Aprili 24, 2026 jijini Dar es Salaam, kituo hicho kilichopo Masaki kinatoa huduma mbalimbali za hali ya juu ikiwemo IVF, IUI, uchunguzi wa vinasaba (genetic testing), pamoja na huduma za kuhifadhi uwezo wa uzazi (fertility preservation).
Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, kituo hicho kimefanikiwa kufanya mizunguko mingi ya matibabu ya uzazi (OPU+FET), hatua iliyochangia kuzaliwa kwa zaidi ya watoto 400 kupitia teknolojia saidizi ya uzazi (ART), ikiwa na kiwango cha mafanikio kinachofikia asilimia 65.
Aidha, NuLife imeendelea kushirikiana na wataalamu wa kimataifa, akiwemo Dr. Nayana Patel, kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kuimarisha teknolojia pamoja na kuongeza ujuzi kwa wataalamu wake wa ndani.
Ushirikiano huo pia unahusisha utoaji wa huduma za upasuaji wa kisasa kwa kutumia matundu madogo (keyhole surgery), unaosaidia kutibu matatizo mbalimbali ya uzazi kama vile uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (fibroids), vifuko vya maji (cysts) pamoja na endometriosis katika hatua zake zote.
Akizungumza kwa niaba ya kituo hicho, mwakilishi wa NuLife alisema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha huduma bora za uzazi zinapatikana kwa watu wengi zaidi huku wakizingatia viwango vya kimataifa.
“Tunajizatiti kuhakikisha tunatoa huduma bora, zenye huruma na zinazomweka mgonjwa mbele, huku tukichanganya teknolojia ya kisasa na utaalamu wa hali ya juu,” alisema mwakilishi huyo.
Mbali na huduma hizo, kituo hicho pia kinatoa matibabu mengine ya uzazi ikiwemo PRP, TESA/PESA pamoja na programu za kuhifadhi viinitete (cryopreservation), na hivyo kuwa kituo jumuishi kinachoshughulikia changamoto zote za uzazi na afya ya wanawake.
NuLife Advanced Fertility Centre inaendelea kuwa chaguo la kuaminika kwa watu wanaotafuta suluhisho la changamoto za uzazi, kwa kuzingatia ubora wa huduma, teknolojia ya kisasa na wataalamu wenye uzoefu mkubwa.





