Na. John Bukuku- Dodoma
Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (MSD) Kanda ya Dodoma, Bi. Mwanashe Juma, amesema kuwa, kwa kushirikiana na Hospitali ya Afya ya Akili ya Milembe, MSD imefanya kikao cha uratibu wa dawa za magonjwa ya akili. Katika kikao hicho, makubaliano ya kuhakikisha upatikanaji wa dawa za magonjwa ya akili katika ngazi zote za huduma yalifikiwa.
Ameyabainisha hayo Aprili 24, 2026 Jijini Dodoma, katika kikao kazi kati ya Bohari ya Dawa MSD na Wahariri wa vyombo vya habari kinachofanyika katika ghala kuu la MSD Kizota.
Aidha, amebainisha kuwa kwa mara ya kwanza, MSD itaanza kuingiza dawa ya Naltrexone, inayotumika kwa watu wanaopambana na uraibu wa pombe. Dawa hii, ambayo inatarajiwa kufika hivi karibuni, itasambazwa kupitia Hospitali ya Milembe na vituo vingine vya kutolea huduma ambavyo vitakuwa vimeainishwa.
Pia ameongeza kuwa wataalamu wa afya ya akili wamesema kuwa uhitaji wa dawa hii ni mkubwa, hususan miongoni mwa walevi, huku akibainisha kuwa MSD itatoa kiasi kidogo cha dawa, lakini kulingana na mahitaji yatakavyoongezeka, kiasi cha dawa kitakachozalishwa kitaongezeka pia.





