IRINGA, 29 Machi, 2026

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), akiambatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, leo amepokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Ismani, Marehemu Mhe. William Vangimembe Lukuvi.

Mwili huo umepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Iringa ukitokea jijini Dar es Salaam baada ya mapokezi hayo, viongozi na mamia ya wananchi wameongoza msafara kuelekea nyumbani kwa marehemu eneo la Gangilonga – Iringa kwa ajili ya taratibu za mazishi na kutoa heshima za mwisho.