Afisa Usalama Mwandamizi TANESCO Mkoa wa Temeke Bw. Stephen Maganga, Afisa Habari, Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Temeke Lucia Renatus wakitoa elimu kwa wakazi wa Kata ya Kijichi, Dar es Salaam  iliyofanyika Machi 5, 2026.

Afisa Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Bw. Goodluck Assenga akitoa elimu kwa mwananchi wa kata ya kijichi, Dar es Salaam.

Afisa Huduma kwa Wateja TANESCO Wilaya ya Mbagala  Verdiana Ndamboba (kulia) akisikiliza maoni ya wananchi wa Kata ya Kijichi wakati  kutoa elimu 

 

Afisa Huduma kwa Wateja TANESCO Wilaya ya Mbagala Bw. Mustapha Hamza (wa pili kutoka kulia) akitoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa umeme.

………..

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke limeendelea kuwafikia wananchi kwa kutoa huduma za moja kwa moja katika maeneo mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa umeme, matumizi sahihi ya mita janja (Smart Meters), pamoja na kupokea maoni na kushughulikia changamoto zinazowakabili wateja, hatua inayolenga kuboresha utoaji wa huduma na kuimarisha uhusiano kati ya shirika na wananchi.

Akizungumza Machi 5, 2026 wakati wa utoaji wa elimu kwa wateja katika Kata ya Kijichi, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Afisa Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Bw. Goodluck Assenga, amesema kuwa lengo la zoezi hilo ni kuwapa wananchi nafasi ya kutoa maoni yao na kupata ufumbuzi wa changamoto wanazokutana nazo katika huduma za umeme.

Bw. Assenga alieleza kuwa TANESCO Temeke inaendelea kusogeza huduma karibu zaidi na jamii ili kuhakikisha changamoto za wateja zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati na kwa ufanisi, huku akieleza utoaji wa elimu hiyo unalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu matumizi sahihi na salama ya umeme.

Aidha, amewahamasisha wananchi kuwasiliana na TANESCO kupitia njia rasmi za mawasiliano wanapohitaji huduma au wanapokumbana na changamoto ambazo ni kupiga simu bure kupitia namba 180 pamoja na kutumia mitandao ya kijamii, ikiwemo WhatsApp, ili kupata msaada kwa haraka.

Kwa ujumla, TANESCO Mkoa wa Temeke imeendelea kuonyesha dhamira ya kuwa karibu na wananchi kwa kusikiliza maoni yao na kushughulikia changamoto kwa haraka, huku ikiendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa umeme.