Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Ahmed Abbas,akitoa taarifa ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo katika Mkoa wa Ruvuma itafanyika  kwenye viwanja vya Tamasha mji mdogo wa Peramiho Wilayani Songea.

Mratibu wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Mkoa wa Ruvuma Xveria Mlimila,akizungumza na Waandishi wa Habari(hawapo Pichani)kuhusu maandalizi ya maadhimisho hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile,akizungumzia maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake ambayo katika Mkoa waRuvuma yatafanyika katika Halmashauri ya Wilaya Songea

………….

Na Mwandishi Wetu, Songea

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Ahmed Abbas amesema, maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yana maana kubwa kwani yanalenga kutathimini utekelezaji wa agenda ya usawa wa kijinsia ,haki na uwezeshaji wa wanawake katika masuala ya maendeleo ya kijamii,kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.

Brigedia Jenerali Abbas, ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo katika Mkoa wa Ruvuma yatafanyika  Wilayani Songea.

Alisema kuwa, ushiriki mpana wa jamii na wadau katika maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani kwa mwaka 2026 yataunganisha nguvu na rasilimali za wadau mbalimbali katika kuhamasisha, kuelimisha na kuchukuwa hatua za pamoja katika kuleta usawa wa jinsia ,haki na uwezeshaji wa wananwake na wasichana.

Abbas alisema, kupitia kauli mbiu ya mwaka huu 2026 inayosema haki na usawa kwa wanawake na wasichana ni msingi Jumuishi kufikia dira 2050 na kwamba kauli mbiu hiyo inalenga kujenga uelewa wa kuwekeza kwenye maendeeo jumuishi.

Aidha alisema,kauli hiyo inatambua haki za wanawake na wasichana na Serikali ya Mkoa wa Ruvuma ithakikisha inafanyiwa kazi kwa vitendo na kuleta mabadiliko ya kweli kama ilivyoainishwa kwenye nguzo ya Dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka  2050.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile alisema, wilaya ya Songea kupitia Halmashauri ya wilaya ya Songea imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwezesha mbalimbali ikiwemo kundi kubwa la wanawake kwa kutoa mikopo iliyowezesha wanawake kuanzisha shughuli za kiuchumi na kujikwamua na umaskini.

Amewataka wanawake wa wilaya hiyo na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla,kutumia maadhimisho ya mwaka huu kuleta bidhaa mbalimbali zikiwemo za kilimo na ususi wa vikapu,mikeka  vyenye hadhi ambavyo vimekuwa kivutia kikubwa kwa  watalii wa ndani na nje ya nchi.

Alisema,wilaya ya Songea ina miradi mingine iliyofanywa na wanawake kwa ajili ya uzalishaji mali na asilimia 10 inayotengwa na Halmashauri kwa ajili ya wanawake imewawezesha kujikwamua kiuchumi husuani katika nyanja za kilimo ambapo katika msimu wa kilimo 2025/2026  wakulima wa wilaya hiyo wamefanikiwa kuuza zaidi ya tani 70,000 za mahindi  na tani 10,000 zimeuzwa nchi jirani ya Zambia.

“ Katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani,wanawake wa wilaya ya Songea wamejipanga kuonyesha bidhaa wanazozalisha wenyewe kama vile mazao ya kilimo,mikeka na vikapu ambavyo vimekuwa kivutio kikubwa vha wageni wanaotoka nje ya wilaya yetu,natoa wito kwa watu mbalimbali waje kwa wingi kwenye viwanja vya furahisha ili kujionea bidhaa za wanawake wajasiriamali”alisema Ndile.

Alisema,lengo mahususi la maadhimisho haya ni kutambua mchango wa wanawake katika Taifa ili na wilaya ya Songea kwa ujumla hasa baada ya  wanawake kuwa ndiyo kubwa linalozalisha  kwa kiwango kikubwa mazao ya chakala na ndiyo wanatunza familia.

Afisa maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma ambayo ni mratibu wa maadhimisho hayo alisema, Xsaveria Mlimila alisema,maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yatafanyika katika   Halmashauri ya wilaya Songea k wenye viwanja vya Tamasha mji mdogo wa Peramiho.