Mkurugenzi wa Habari Maelezo Zanzibar Salum Ramadhan Abdalla akitoa hotuba ya Makaribisho katika Mkutano wa Waandishi wa Habari na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk,Khalid Salum Mohamed akizungumzia Maendeleo na Mafanikio ya Wizara yake kufikia Siku Mia Moja za Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK,Hussein Ali Mwinyi toka kuchaguliwa kwa kipindi cha Awamu yake ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk,Khalid Salum Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maendeleo  na Mafanikio ya Wizara yake kufikia Siku Mia Moja za Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK,Hussein Ali Mwinyi toka kuchaguliwa kwa kipindi cha Awamu yake ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk,Khalid Salum Mohamed akifafanua Jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maendeleo  na Mafanikio ya Wizara yake kufikia Siku Mia Moja za Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK,Hussein Ali Mwinyi toka kuchaguliwa kwa kipindi cha Awamu yake ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk,Khalid Salum Mohamed akisisitiza  Jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maendeleo  na Mafanikio ya Wizara yake kufikia Siku Mia Moja za Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK,Hussein Ali Mwinyi toka kuchaguliwa kwa kipindi cha Awamu yake ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar.

Mwandishi wa Habari kutoka ZBC Amina Mchezo akiuliza Maswali katika Mkutano wa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk,Khalid Salum Mohamed na Waandishi wa Habari akizungumzia Siku Mia Moja za Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK,Hussein Ali Mwinyi toka kuchaguliwa kwa kipindi cha Awamu yake ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Rahaleo Zanzibar. (PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR.02/03/2026)

…………….

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Imeanza maandalizi ya ujenzi wa Barabara ya Tunguu hadi Makunduchi  yenye urefu wa kilomita 48 ambapo hatua za ujenzi huo umeshakamilika.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Khalid Mohamed Salum kuhusiana na siku 100 za Mafanikio ya uongozi wa awamu ya pili ya Dkt. Mwinyi amesema ujenzi huo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi wa kuimarisha miundombinu ya usafiri.

Amesema ujenzi huo utahusisha njia nne, na kuwekwa taa kuanzia Tunguu hadi Mkunduhi ili kuimarisha usafiri na kuwaondoshea wananchi usumbufu na unatarajia  kuanza wakati wowote na wakandarasi wa ujenzi wameshakamilisha maandalizi ambapo utajengwa na Kampuni ya MECCO.

Aidha amesema kuwa barabara ya Fumba hadi Kisauni yenye km 12, Mkoani hadi Chakechake tayari maandalizi yake yameshakamilika na ujenzi wake unatarajiwa kuanza ili kuweza kukuza Uchumi na kuleta maendeeleo nchini.

“Ujenzi wa Barabara hizi utakapokamiliza utaweza kuleta maendeleo na kukuza uchumu wa nchi na kukuza kipato kwa wananchi”, ameeleza Waziri Khalid.

Akizungumzia kuhusiana Bandari ya Mpigaduri Dkt. Khalid amesema kuwa ujenzi wa bandari hiyo itabadilisha muonekano na kuweka haiba nzuri katika maeneo hayo ili kuendelea kuiletea nchi maendeleo ambapo bandari hiyo itajumuisha bandari tatu ikiwemo ya vyombo vya baharini kwa ajili ya abiria, bandari kuu ya ndege za baharini kwa ajili ya kukuza utalii pia ni kituo cha tax ya ndege za baharini.

“Bandari ya Mpigaduri itakuwa ni bandari ya kisasa ambayo itakuwa na muonekano wa kuweka haiba nzuri katika eneo hilo kwa kukuza na kuleta maendeleo kwani itajumuisha bandari tatu ikiwemi bandari ya ya vyombo vya abiria, bandari kuu ya ndege baharini na kituo cha tax ya ndege za baharini (water tax) na kuweka kituo cha mabasi ili kuondosha mongamano wa usafiri.  

Aidha ameeleza kuwa meli ya MV Mapinduzi II itaanza kazi zake za usafirishaji wa wananchi mizigo mwezi ujao Machi ili kuondosha usumbufu baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa.

Hata hivyo Dkt. Khalid amefahamisha kuwa serikali inatarajia kuweka usafiri wa njia ya reli ili kukuza utalii na kuimarisha usafiri kwa lengo la kukuza mapato na kuboresha maendeleo na kurejesha usafiri huo ambao ulikuwepo na kutumika hapo zamani.

Waziri Khalid amesema kuwa Serikali imeweka mkazo katika kudhibiti usalama barabarani katika kulinda maisha ya watu kwa kuwadhibiti madereva wazembe waaokiuka sheria za nchi na kutoa mafunzo kwa viongozi wa dini pamoja na kuweka CCTV katika baadhi ya Barabara.

Waziri amefahamisha kuwa serikali tayari imeshalipa zaidi ya sh. Bilioni38 kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wananchi waliopitiwa na ujenzi wa miradi ya maendeleo katika maeneo ili kuondosha usumbufu na kuleta mafanikio nchini.   

Aidha amewataka wananchi kucha tabia ya kujenga karibu na Barabara ili kuepusha hasara na madhara wakati wa ujenzi unapoendelea pamoja na kukubali kubadilika katika kuleta maendeleo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kasi ya maendeleo ya awamu ya pili Dkt. Mwinyi.