_β–ͺ️Mkutano huo unafanyika katika hoteli ya Ngurudoto-Arusha, Februari 24, 2026_

πŸ“Œ Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwamua miradi iliyoshindwa kutekeleza kwa muda mrefu na ameibua miradi mipya katika maeneo ambayo yalikosa maji kwa muda mrefu.

πŸ“Œ Tunatakiwa tushinde β€˜Site’, pale ambapo fedha ipo na wananchi wanahitaji maji, hatutakiwi kuchelewesha hata kwa nusu saa maji ambayo yalitakiwa yawe yameshapatikana, kupanga maisha bila maji ni jambo gumu sana.

πŸ“Œ Jambo la kutunza vyanzo vya maji liwe ni jukumu la kila mtu, jambo hili lichukuliwe kuwa ni jambo la kiusalama, tukichezea vyanzo vya maji hata kama fedha zipo tutakosa maji.

πŸ“Œ Si jambo zuri kusikia wananchi wanakosa maji halafu kuna mahali maji yanapotea, kagueni miundombinu yetu ya usambazaji wa maji ili tukomeshe upotevu wa maji.

πŸ“Œ Kwa maono ya kiuongozi, Rais Dkt . Samia Suluhu Hassan katimiza wajibu wake kwa kununua mitambo kwenye mikoa yetu nchini na kila ukanda kuna mtambo wake wa kuchimba na kupata maji.

πŸ“Œ Mkoa wowote ambao wananchi watalalamika kuhusu kukosa maji ni sisi kwenye mamlaka za maji tutakuwa tunakwamisha, tumieni magari na mitambo ya kupimia maji mliyopewa ili wananchi wapate maji, tunataka tuwape tabasamu Watanzania, Maji hayana mbadala.

πŸ“Œ Tunataka kila shule ya msingi na Sekondari, Zahanati, vituo vya afya viwe na maji, inaweza kuwa mradi au kisima. Mitambo tunayo hivyo tunapaswa kwenda kulifanya hilo litokee.

πŸ“Œ Utunzaji wa vyanzo vya maji si jambo la Mamlaka za maji pekee, si la Wizara ya Maji pekee, si la Wizara ya Maliasili na Utalii pekee, ni jambo la kila mtanzania, tunatunza uhai wetu tunapotunza vyanzo vya maji.

πŸ“Œ Naridhishwa na kazi kubwa katika sekta ya maji, tumeshapiga hatua kubwa sana katika kuwapa maji watanzania, twendeni tukamalizie palipobaki.