MKURUGENZI mkuu wa bodi ya sukari Tanzania ,Profesa Kenneth Bengesi akizungumza jijini Arusha kuhusiana na huduma wanazotoa .

Happy Lazaro,Arusha .

Arusha .MKURUGENZI mkuu wa bodi ya sukari Tanzania ,Profesa Kenneth Bengesi amesema kuwa ,Mifumo ya Tehama imesaidia na imeleta mabadiliko kwa kiasi kikubwa sana tofauti na kipindi cha nyuma ambapo kulikuwa na udanganyifu mkubwa wa vibali feki ila kwa sasa hivi hilo limekufa kwa sababu ya kutumia mifumo ya kitehama .

Kwa kutumia mifumo ya Tehama.imetengeneza mazingira salama kwamba mtu yoyote anaweza kujiridhisha kuwa kibali.anachopewa kipo sahihi kwani vibali vyote vina alama za kiusalama ambao vimewekewa .

Aidha bodi ya Sukari Tanzania ni kati ya Taasisi za umma ambazo zinatumia sana mifumo ya Tehama kwenye usajili wa wakulima wote ambao wanalima kilimo.cha miwa kwa kuzalisha sukari wamesajiliwa na wanatumia mfumo ambao unaenda kuwasajili wakulima na kutambuliwa .

Profesa Bengesi ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizungumza kwenye kikao.kazi cha sita cha serikali mtandao kilichofanyika jijini Arusha .

“Kupitia mfumo wa Tehama Mkulima hawezi kutumia shamba lake kukopea mara mbili ukishalikopea huwezi kulikopea tena na hiyo inahakikishia taasisi za fedha kuwa hela yake wanayoitoa na mkulima aliyekopa na kuweka shamba lake kama dhamana mkopo wake upo salama tofauti na siku za nyuma ambazo shamba moja linaweza likakopewa na wakulima wawili ama watatu wakija kulipa anakamatwa mwenye shamba ambapo benki zilikuwa zinapoteza fedha zao ila kwa sasa hivi tatizo limetatuliwa kwa kiwango kikubwa sana .”amesema Profesa Bengesi. 

Aidha amesema kuwa wakulima wanapokuwa wamesajiliwa inawawezesha kuwa na uhakika wa soko la bidhaa yao wanayozalisha kwa maana ya miwa kwani wanaingia mikataba na viwanda vinavyozalisha sukari na ili uweze kuingia mkataba na viwanda vinavyozalisha sukari ni laizma uwe umesajiliwa na bodi ya sukari na uingie mkataba unaokutambulisha na unakuwa umenicomite kuwa sukari unayozalisha kiwanda kinainunua hivyo manufaa wapo kwa pande zote mbili.

“Lengo la bodi ya sukari ni kuhakikisha kuwa kila mdau kiwanda hakimwonei mkulima na mkulima naye apate faida ambayo hatapata hasara katika kilimo chake cha miwa na hiyo inajenga mazingira mazuri sana kwa wote .”amesema Profesa .

Ameongeza kuwa ,kuna manufaa mengi ambayo wananufaika nayo kwa kutumia mfumo wa Tehama ambazo zinatolewa na serikali mtandao .

“Ukiangalia hata huduma tunazotoa kwa wateja wetu kwa mfano waigizaji wa matumizi ya viwanda zamani mteja akihitaji sukari alikuwa akisafiri na document aje kuwasilisha ofisini zianze kuchakatwa na ilikuwa inachukua muda mrefu sana inaweza kuchukua hata wiki lakini pia gharama za usafiri toka mwanza au mikoani kuja kufuata huduma ila kwa sasa hivi shighuli zote hizo zinafanyika.kwenye mtandao akiwa ofisini kwake au hata kwa njia ya simu yake ya mkononi kila kitu anafanya na anapata kibali.chake ndani ya siku moja .”amesema Profesa . 

“Wanatumia pia kwa matumizi ya ofisini ya “E office” ambayo inatumika kuhudumia huduma za kiofisi zote na ni kitu ambacho kinaenda kwa dakika moja na ikikwama unajua imekwama kwa ofisa gani na ile inarahisisha kwanza kuweka uwazi kwa namna wanavyotoa huduma zao na inaimarisha uwajibikaji tofauti na huduma za mafaili maana huwezi kujua hata file limepotelea wapi tofauti na sasa hivi kwani ni rahisi kufuatilia na kupata huduma kwa wakati .

Bodi ya sukari Tanzania ni moja ya taasisi za serikali ambayo ina majukumu makubwa matano ikiwemo kufanya udhibiti kwenye tasnia ya sukari katika kuhakikisha kuwa wadau katika mnyororo mzima wa sukari wanaweza kufuata masharti ya kisheria ambayo yatawezesha wadau wote kuja kufanya biashara zao kwa tija.

Amesema kuwa kuwa jukumu la pili ni kuendeleza tasnia ya sukari kwa maana ya kusimamia maslahi ya wadau wote na kuwapa sapoti pale wanapohitaji kwa ajili ya kuwa na uendelevu katika sekta ya sukari .

“Tunasimamia maslahi wa wadau wengine kama.vile taasisi za fedha tunapokuwa tumedhibiti mazingira ya biashara kuwa mazuri ambayo yanakuwa na manufaa kwa walaji na kwenda viwandani ili wanaozalisha sukari waweze kufanya biashara yao kwa tija na wakati huo tunakuwa tunawahakikishia taasisi za fedha kuweza kurejesha mikopo yao ambayo wanatoa kwa wadau katika mnyororo wa dhamani kwani taasisi za benki zimekuwa zikitoa mikopo kwenye viwanda kwa ajili ya kufanya upanuzi au kwa wawekezaji wanaojenga viwanda vipya na kwenye kilimo kwa maana ya walulima wanaotaka kulima kilimo cha miwa ambayo baadaye inasindikwa kwa ajili ya kuzalisha sukari.”amesema .

Ameongeza kuwa majukumu mengine ambayo wamekuwa wakifanya ni kusaidia ukuaji wa teknolojia katika tasnia ya sukari ambapo wanawekeza kwenye utengenezaji wa teknolojia ambazo zinasaidia wakulima wadogo na wadau wengine kwenye mnyororo wa dhamani .

“Kama hivi sasa tumewekeza kwenye utengenezaji wa kiwanda kidogo na Temdo ambapo kiwanda hicho kidogo kitakuwa kinaweza kuzalisha sukari na kitakuwa kinasimikwa kwenye maeneo ambayo yana uwezo wa kuzalisha na kulima miwa ambayo itaongeza kwenye pato la Taifa la sukari.”amesema .