Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 20, 2026 amemjulia hali mbunge wa Moshi Mjini Mhe. Ibrahim Shayo ambaye amelazwa katika hospitali ya KCMC iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro. Mhe. Ibrahim alipata ajali Februari 18, 2026 katika eneo la Kirinjiko, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. Pembeni ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Florence Samizi. 

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Mabogini, Wilaya Moshi Mkoani Kilimanjaro Mara baada ya kutembelea ujenzi wa barabara ya Spencon-Mabogini-Kahe-Chekereni yenye urefu wa kilomita 31.25 leo tarehe 20 Februari, 2026.. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi katika eneo la Chekereni mkoani Kilimanjaro akiwa anaendelea na ziara zake za kikazi mkoani humo leo tarehe 20 Februari, 2026. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akiweka jiwe la msingi la jengo la Halmashauri ya Moshi mkoani kilimanjaro leo tarehe 20 Februari, 2026.  PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Muonekano wa Jengo la Halmashauri ya Moshi mkoani kilimanjaro lililozinduliwa rasmi leo tarehe 20 Februari, 2026 na Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU