Aliyeko kulia ni Mrajis mkuu wa vyama vya ushirika nchini,Dkt.Benson Ndiege akitoa maelezo mbele ya Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.Moses Kusiluka alipotembelea banda hilo jijini Arusha .
……..
Na Happy Lazaro,  Arusha
Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) imeonesha ubunifu mkubwa katika kusimamia vyama vya ushirika, ambapo imepokea  pongezi kutoka kwa Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi, wakati akifungua kikao kazi cha sita cha  Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kinachoendelea Jijini Arusha.
Balozi Kusiluka amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ulinzi na usalama wa taarifa binafsi, huku akieleza kwamba taasisi zote zinapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni, na Viwango vya Serikali Mtandao.
Mrajisi wa Vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, aliwasilisha maelezo ya kina kuhusu mfumo wa kisasa wa usimamizi wa vyama vya ushirika katika banda la maonyesho.
Aidha akitoa wasilisho lake mbele ya Katibu Mkuu  Kiongozi ,jinsi TCDC inavyotumia teknolojia za kidijitali kuongeza uwazi, kuboresha uwajibikaji, na kurahisisha utendaji wa taasisi ambapo amesema Mfumo huo unarahisisha maamuzi ya ushirika na kuhakikisha taarifa zinapatikana kwa wakati.
Balozi Kusiluka ameongeza kuwa mfano wa TCDC unapaswa kuigwa na taasisi nyingine zinazojihusisha na TEHAMA katika sekta ya umma.
 Amefafanua kuwa taasisi zinazoshindwa kufuata miongozo ya usalama na usimamizi wa taarifa lazima zichukuliwe hatua, ili kuhakikisha uwazi na ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za e-Gov
“Shughuli za kikao cha Serikali Mtandao zinaendelea Jijini Arusha, zikitoa fursa kwa wadau wa sekta ya ushirika kujifunza, kubadilishana uzoefu, na kuendeleza utumiaji wa teknolojia katika taasisi za umma”amesema .