Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dkt. Islam Seif Salum ambaye ni Mwenyekiti akiongoza kikao cha ushirikiano baina ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, ngazi ya Makatibu Wakuu kilichofanyika Zanzibar leo Februari 16, 2026. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi ambaye ni Mwenyekiti Mwenza akizungumza wakati wa kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, ngazi ya Makatibu Wakuu kilichofanyika Zanzibar leo Februari 16, 2026

Wajumbe wakifuatilia kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, ngazi ya Makatibu Wakuu kilichofanyika Zanzibar leo Februari 16, 2026.