Afisa michezo wa Halmashauri ya wilaya Mbinga Mkoani Ruvuma Charles Maero kushoto,akipokea jezi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Joseph Kashushura(hayupo pichani)kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kamapuni ya Wailes ya Mbinga Frank Ndunguru kulia, baada ya kumalizika kwa bonanza kubwa la michezo lililowakutanisha wananchi,watumishi na madiwani wa Halmashauri hiyo(Picha na Muhidin Amri)
Baadhi ya watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga Mkoani Ruvuma,wakifanya mazoezi ya viungo,wakati wa bonanza kubwa lililoandaliwa kwa ajili ya watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye viwanja vya jengo la kitega uchumi la Mbinga Dc Mall.(Picha na Muhidin Amri)
………….
Na Mwandishi Wetu, Mbinga
Wananchi wa Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma,wamehimizwa kufanya mazoezi mara kwa mara na kupunguza kula vyakula vya mafuta ili kuepukana na magonjwa yasioambukiza.
Ushauri hui umetolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Jogging Wilaya ya Mbinga Ibrahim Ali,wakati akihitimisha mazoezi ya pamoja yaliyowashirikisha wananchi, watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga kwenye viwanja vya Mbinga Dc Mall.
Alisema, mazoezi yana faida nyingi kiafya ikiwemo kuzia uwezekano wa kupata magonjwa kama vile shinikizo la damu,presha,kisukari,saratani na magonjwa ya moyo ambayo ni hivi sasa yamekuwa changamoto kubwa hapa nchini.
Alisema,njia pekee ya kuepuka kupata maradhi hayo ni kushiriki kufanya mazoezi.
Alisema,sehemu kubwa ya watu wanaopata magonjwa hayo yanasababishwa na kutofanya mazoezi ya mara kwa mara,kwa hiyo ni vema watu washiriki mazoezi hususani ya viungo ili kulinda afya zao na kuepuka kupata magonjwa yasioambukizwa.
Naye Diwani wa viti maalum kata ya Kihangimauka Leonora Mwinuka,ameiomba Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga kuhakikisha suala la mazoezi linapewa kipaumbele na lifanyike mara kwa mara kwa kuwa linasaidia sana kulinda afya zao.
Mwinuka ambaye ni Mwenyekiti wa Madiwani wanawake wilaya ya Mbinga alisema,mazoezi yanafaida mbalimbali ikiwemo watumishi kufahamiana na watu mbalimbali madiwani na wananchi wa kawaida na kuungana katika kuleta maendeleo ya Halmashauri ya wilaya Mbinga.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Joseph Kashushura,Afisa michezo wa Halmashauri ya wilaya Mbinga Charles Maero alisema,mazoezi hayo ni sehemu ya Bonanza lililowajumuisha watumishi, madiwani na wananchi kutoka sehemu mbalimbali ya Mbinga wakiwemo watumishi wa Halmashauri ya Mji Mbinga.
“lengo lingine la kufanya la kuaanda Bonanza hili ni kujenga urafiki na kumarisha afya za wananchi pamoja na kuleta ushindani kati ya watumishi wa idara moja na nyingine,watumishi kufahamiana na kujenga urafiki na wananchi wa kawaida”alisema Maero.
Katika Bonanza hilo michezo mbalimbali ilifanyika ikiwemo washiriki kutembea kilometa tano kutoka uwanja wa michezo wa CCM,kucheza mpira wa miguu,pete na kukimbia kwenye magunia,mchezo wa wavu,mbio za kufukuza kuku,pool table,karata,bao na riadha na washindi walikabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo kombe na medali.
