………….

Licha ya Ukuaji wa Sayansi na Teknolojia Watumishi wa Umma hawana budi Kutumia akili matumizi Mnemba (Unde) (AI) katika kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi ili kuendana na Kasi ya Dunia

Daudi ameyasema hayo Jijini Dar es salaam mapema Februari ,2026 na NAIBU Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Xavier Daudi wakati akifungua mdahalo kuhusu matumizi ya akili Mnemba(AI) katika kuboresha huduma kwa umma ulioandaliwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania ( TPSC).

“Serikali imejipanga kikamilifu kutumia Teknolojia ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence – AI) ili kuongeza ufanisi, kasi na ubora wa utoaji huduma kwa wananchi, kufuatia mabadiliko makubwa ya kidunia katika sekta ya teknolojia”Amesema Daud

Amesema pamoja na Serikali kuendelea kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika miaka ya hivi karibuni, ukuaji wa kasi wa teknolojia ya Akili Mnemba umeleta mazingira mapya yenye changamoto na fursa katika utumishi wa umma, hivyo ni muhimu kuendana na mabadiliko hayo.

“Ni dhahiri kuwa mabadiliko ni makubwa katika mazingira na kasi ya ukuaji wa teknolojia. Hatuwezi kubaki nyuma wakati dunia inakwenda kwa kasi. Nasi Serikalini tunapaswa kutumia teknolojia ya akili mnemba kuhakikisha wananchi wanafaidika na huduma zinazotolewa kwa haraka na kwa ufanisi zaidi,” amesema Daudi

Ameeleza kuwa matumizi ya teknolojia hiyo yataisaidia Serikali kupata majawabu sahihi kwa wakati, kutatua changamoto za wananchi kwa ufanisi na kuwafikia kwa wakati muafaka.

Aidha, amesisitiza kuwa Serikali haijakaa kimya katika suala hilo, bali tayari imeanza kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha mifumo ya utoaji huduma kwa kutumia teknolojia za kisasa, akitolea mfano eneo la ajira ambapo mifumo ya kidijitali imeanza kutumika kuboresha mchakato huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania(TPSC),Dkt.Ernest Mabonesho ,amesema matumizi ya Akili Mnemba (AI)katika utumishi wa umma ni hatua muhimu itakayorahisisha utoaji wa huduma na kuongeza ufanisi kwa watumishi.
‎
‎Dkt.Mabonesho amebainisha kuwa ingawa akili Mnemba ni dhana mpya katika utumishi wa umma, ni teknolojia ambayo haiwezi kuepukika.

‎“Hii ni teknolojia ambayo inalazimisha tuanze kuitumia kwa sababu inaleta wepesi katika utoaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza uwazi pamoja na ufanisi,” alisema.


‎
Nae mshiriki wa mdahalo huo,Mahyolo Kalokola,amesema mjadala huo umemfungua macho kuhusu fursa zilizopo katika matumizi ya Akili Mnemba.