WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa TANESCO Ndg. Lazaro Twange, kuhusu Mradi wa kupooza umeme uliopo Mkata mkoani Tanga  pamoja na ujenzi wa njia za kusambaza umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 45 kutoka kituo cha Mkata kwenda kijiji cha Kwamsisi wakati alipoweka jiwe la msingi wa Mradi huo leo Februari 13, 2026. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU.

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba akiweka jiwe la msingi wa Mradi wa kupooza umeme uliopo Mkata mkoani Tanga  pamoja na ujenzi wa njia za kusambaza umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 45 kutoka kituo cha Mkata kwenda kijiji cha Kwamsisi leo Februari 13, 2026. kutoka kushoto ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Meneja wa TANESCO Ndg. Lazaro Twange, Mwenyekiti CCM Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdallah, Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, Mkuu wa Mkoa Tanga, Dkt. Batilda Buriani, Waziri wa TAMISEMI, Prof. Rizaki Shemdoa,Waziri wa mifugo na uvuvi, Dkt. Bashiru Ally. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU.

PMO_2388

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Februari 13, 2026 akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa mahuituti (ICU) katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Handeni mkoani Tanga. Ujenzi wa Jengo hilo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 426. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

 

PMO_2415

 

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, akizungumza na baadhi ya Wauguzi katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Handeni mkoani Tanga mara baada ya kutembelea Hospitali hiyo na kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa Jengo la Wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali hiyo leo Februari 13, 2026.  PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

 

 

PMO_2565

 

Baadhi ya Wananchi wakiwasilisha changamoto zao kwa Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati wa Mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Handeni Square mkoani Tanga leo Februari 13, 2026.  PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

 

 

PMO_2526

 

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, akizungumza katika mkutano wake wa hadhara na Wananchi wa Handeni katika Uwanja wa Handeni Square mkoani Tanga leo Februari 13, 2026.  PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU