Biashara ya M-Pesa ina changamoto zake, na kubwa zaidi ni utapeli au kutuma pesa kimakosa kwa namba isiyo sahihi. Hiki ndicho kilichomkuta Sarah, mama wa watoto wawili na wakala wa M-Pesa jijini Nairobi, ambaye nusura afunge biashara yake baada ya kutuma Ksh 60,000 kimakosa kwa namba ya mtu asiyemjua.

Ilikuwa ni siku ya Jumanne yenye pilikapilika nyingi, Sarah alipokuwa akimhudumia mteja aliyetaka kuweka pesa. Kwa bahati mbaya, alikosea tarakimu moja na pesa hizo zikaenda kwa mteja mwingine ambaye alikuwa huko Kisumu. Mara moja, Sarah alipiga simu kwa huduma ya wateja ya Safaricom ili kuzuia muamala huo, lakini aliambiwa kuwa mpokeaji alikuwa ameshatoa pesa hizo zote sekunde chache baada ya kuzipokea na simu yake imezimwa……. SOMA ZAIDIĀ