Kamati ya Kusimamia Uchaguzi wa Baraza la Vijana imetakiwa kufanya KAZI kwa adilifu   na kuacha kupokea ushawishi wa aina yeyote ili kutekeleza majukumu ufanisi
Akifungua mafunzo Elekezi kwa wajumbe hao katika Ukumbi wa Skuli ya Afya (Shaa) Mombasa kwa Mchina  Wilaya ya Magharibi B’ Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Mhe Shaaban Ali Othman amesema kuwa wajumbe hao watafanyiwa Uchunguzi wa kina kwa kufanya mjadala wa wazi ili kufahamu namna gani wanaweza kuwasaidia vijana
Aidha ameitaka Kamati hiyo kuaanda mpango kazi utakaowaongoza katika Kusimamia Uchaguzi huo kwa Ngazi ya  Wilaya na Taifa ambao utaleta tija kwa Vijana na kuwapatia viongozi bora.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Salama Mbaruok Khatib amewataka vijana Kusimamia ipasavyo ili Uchaguzi huo ifanyike kwa salama na Amani
Aidha amewaasa kuwa waadilifu kwani uwezo wa kufanya KAZI wanao na kutegemea kupata viongozi wazuri Wenye sifa.
Akitoa Maelezo kuhusu miundo ya wapiga kura  Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana  Ali Haji Hassan amefahamisha kuwa kijana lazima awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 32 ambae ana kitambulisho cha mzanzibar