Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. John
Magufuli akiwa ameshika dafu alilonunua kwa mfanyabiashara
wa madafu katikati ya jiji la Dar es Salaam. Wanyabiashara na
wajasiriamali mbalimbali wana fursa ya kujikomboa kiuchumi
kama watatumia sehemu ya faida zao kuiwekeza ili kukuza
mitaji yao, kuanzisha biashara kubwa na kutoa ajira.
Familia nyingi zinapokuwa na ahueni ya maisha hupendelea kula chipsi kuku ambazo ni gharama kubwa. Pesa hiyo kama ingewekezwa itakuwa na msaada mkubwa kwa familia ambayo itapata faifa, kukuza mtaji, kuanzisha biashara kubwa.
****************************
Na Mwandishi Wetu
FAMILIA za Kiafrika mara nyingi zimekuwa na wanafamilia
wasiopungua wanane. Hiyo ni staili ya maisha hasa pale familia inapukuwa na ahueni ya kipato japo kidogo.
Utakuta familia kama hizo zina utamaduni wa kudekeza watoto, utasikia kanunueni chipsi kuku, watoto utawasikia wakisema sisi hatupendi ugali, maharage, mchicha na mtindi.
Maharage ndio usiseme kabisa, utamsikia mama akiwauliza watoto sasa mtakula nini? jibu rahisi la watoto utawasikia wakisema chipsi kuku au chipsi zege (mayayi) na kuku.
Kwa sasa kilo ya unga sh. 1,000, mnakula wote tena zaidi ya mlo mmoja, chips kuku sh. 5,000 au zaidi na hamuwezi kula wote. Mkiwa zaidi ya watu 8, chipsi mayai na kuku ni pesa nyingi, mkila mara kwa mara ni pesa nyingi zaidi.
Fedha hizo zingeweza kuwekezwa. Kiafya ugali na maharage, mchicha na mtindi ni bora zaidi kuliko chipsi kuku.
Unapokula chipsi, mayai na kuku kila mara, muda nao
hausubiri, kadri unavyokwenda uzee nao unabisha hodi.
Kama ulizaa watoto miaka kadhaa iliyopita, watoto hao
wanatakiwa kwenda sekondari au chuo. Umri wa mzazi
unakwenda na kuwa watu wazima zaidi ambao kimsingi
watahitaji uangalizi.
Pesa zote zikiishia kwenye chips kuku bila kufikiri kesho yake I changamoto kubwa, chipsi, mayai na kuku imeleta shida katika familia nyingi na mwisho wa siku kusababisha umaskini.
Ukiwa kwenye umri wa kati inabidi uhudumie watoto na
familia, inawezekana wazazi wako pia wanakutegemea, hizi ndizo tamaduni za familia za kiafrika.
Pengine wote tupo humo na maisha yetu yako taabani, mambo yanakwenda kombo. Ili muda gharama kama hizo kuna jinsi au jambo fulani lazima tulifanye ili tusikonde kwa mawazo na kuyafikiria maisha.
Vuta pumzi twenda pamoja, chunga pesa zako, kumbuka kuna midomo mingi inahitaji uilishe na si kulisha tu lakini na shida zingine za maisha kama mavazi, maradhi hata malazi.
Mambo mengine zaidi ya hayo ni pamoja na kwenda ufukweni, mgahawani na shida za ki ukoo. Afrika mtoto wa mwenzio ni wako pia.
Tukiwa kwenye ndege kukawa na dhoruba marubani na
wahudumu wanasisitiza ujiwekee mwenyewe hewa ya ‘oxygen’ baada ya hapo ndipo umwekee na jiraniyako ili naye aweze kupumua.
Kwa maneno mengine ni kwamba, anza na wewe mwenyewe kwanza halafu jirani kufuatie, jirani anaweza kuwa baba yako, mwanao hata dada au kaka yako wa kuzaliwa tumbo moja.
Mfano kama una madeni, unahagaika kukidhi mahitaji yako
muhimu utayari wako wa kusaidia watu mwingine kifedha
unakuwa bado, inabidi wasubiri, pengine sana.
Kwa kipato chochote unachopata jaribu kuweka kiasi hata
kidogo kwa ajili ya dharura, lipa madeni yako kwa mpangilio maalumu, weka kiasi hata kidogo kama akiba ya uzeeni huku ukikumbuka iko siku watoto wataenda sekondari au chuoni, pamoja na ugumu wa maisha pambana na hali yako.
Wanaokuzunguka waambie ukweli kuwa huwezi watimizia,
acha wakuchukie lakini kama ni chipsi kuku wajifunze kutafuta kwa jasho lao.
Wale wanaokutegemea waende kwa bajeti yako si kwa
matamanio yao, wabane waambie ukweli ili uweze kupata ziada kwa ajili ya uwekezaji.
Wanaoweza kufanya kazi watafute hata vibarua, mfano wakati watoto wanasubiri matokeo ya mitihani na nyakati za likizo au baada ya kumaliza chuo ili waongeze pato la familia.
Kwa kuwa tatizo ni pesa na jinsi ya kuitengeneza, tuongelee pesa mara kwa mara katika usawa wa familia zetu.
Uliza kama watoto, ndugu chini ya familia yako wana madeni na yalikuwa ya nini? Je, kila mtu ana bima ya afya maana maradhi yatakutoa kwenye malengo yako, pesa yote inaweza kuishia kwenye matibabu ya kutibu maradhi.
Kama huna Bima ya Afya unaweza kutumia hadi thumuni ya mwisho nap engine ukaingia hata kwenye madeni badala ya kuwa mwekezaji ukawa fukara wa kutisha.
Kwa watoto waambie ukweli kuhusu maisha, waambie maisha si rahisi na si chipsi, maya na kuku ila yaweza kuwa rahasi kama watakuwa wawekezaji, kuwekeza sehemu sahihi kama kwenye Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja ya UTT AMIS.
Mifuko hiyo, hata unapokuwa na pesa kidogo unaweza kuwa mwekezaji na ukawekeza mara kwa mara kadri unavyopata na inatoa faida jumuishi hivyo mtaji wako na faida kukuwa vizuri kadri miaka inavyosonga mbele.
Ukifanya hivyo utakuwa umewapa watoto wako upendo wa
kweli na si chipsi, mayai na kuku. Kila mtu ni muhimu, hakuna mwenye umuhimu kama baba, mama na watoto.
Mbali na umuhimu huo, kila jambo lina mtizamo na ufumbuzi tofauti kwani usipoangalia utatuzi kwa umakini wapendwa wako kama hao wanaweza kuwa chanzo cha mdororo wako kiuchumi.
Kama wanakutegemea sana, kaa panga nao angalia mpango upi utakuwa mzuri na utakuwezesha kuendelea na maendeleo yako ya kiuchumi vinginevyo mtakufa wote.
Ondoa hisia, angalia kila jambo kiuhalisia, tumia mifano halisi ambapo kwa kufanya hivyo si ukatili ni kwa nia njema kwani uchumi wako ndiyo uchumi wao.
Wekeza kwa bidii, pia ni vizuri kuanza kuwekeza ukiwa bado kijana, kumbuka kuna siri kubwa sana kati ya uwekezaji na muda hasa unapopata faida jumuishi Katika Mifuko UTT AMIS.
Kumbuka japo thamani ya kipande inapanda na kushuka au inaendeana na thamani ya mifuko bado ukianza mapema utakuwa vizuri kiuchumi miaka ya mbele.
‘Ukiwekeza sh. 200,000 kwa mwezi utakuwa umeweka sh.
24,000,000 kwa miaka 10. Kama pesa hizo zitakuwa kwa riba ya asilimia 10 kwa mwaka utakuwa na sh. 40,968,995.78.
“Kama riba ikawa asilimia 12, uwekezaji wako utakuwa sh.
milioni 46,007,737.9 ndani ya miaka 10. Kama uwekezaji huo ukawa wa miaka 20, utakuwa umeweke sh. 48,000,000 kwa asilimia 10 utakuwa na sh.151,873,767.20 kama asilimia ni 12 utakuwa na sh. 197,851,073.08,” anafafanua Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga.
Anasema hayo ndiyo maajabu ya uwekezaji kupitia mifuko ya uwekezaji wa pamoja. Kumbuka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) inasisitiza kueleza ukweli kuwa thamani ya kipande inaweza kupanda au kushuka.
Kumbuka kupanda na kushuka kwa thamani ni tabia ya
uwekezaji wote, hata ungekuwa na duka, hoteli kuna siku unapata zaidi na kuna siku unapata kidogo kwa uwekezaji huo huo au pale unapokuwa umeongeza mtaji.
Ni muhimu jamii ikatambua kuwa kuna dharura hivyo weka fungu la dharura, ikishapatikana wekeza la malengo ya baadae ikiwemo kustaafu, malengo ya kustaafu yanatakiwa yaanze siku ya kwanza unapoanza kazi, punguza chipsi, mayai na kuku.
Mbaga anasema malengo ya baadae sio kustaafu tu, elimu kwa watoto nayo imo, fikiria wakifika chuo itakuwaje, wakifikisha miaka ambayo wanaweza kufanya kazi wasome huku wakifanya kazi ambayo si lazima iwe ya ajira.
Mfano, nyumbani mnaweza mkawa mnafuga mifugo kama
kuku, ng’ombe, mbuzi na mingine, badala ya kuaajiri mtu wa kuhudumia mifugo hiyo ni vizuri watoto wakapangiana zamu.
Pesa ambayo ungemlipa mfanyakazi kwa kazi hiyo inaweza
kuwekezwa kwa maisha ya baadae, kumbuka sh. 1,000,000 ikikaa ndani ya uwekezaji miaka 30 kwa kwa asilimia 15 itakupa sh. 66,000,000, je, ingekuwa milioni mbili, tatu, nne, wakati wa likizo ndefu watoto wanaweza ongeza tija zaidi.
Watoto waishi kwa gharama za bwalo za chuo na si kwa chipsi, kuku na mayai. Hii itawasaidia kuishi maisha halisi na si maisha ya kuiga baada ya chuo.
Ili uweze kuwekeza, wapeleke watoto shule ambazo unaweza kumudu gharama zake, kwa mfano hapa nyumbani kuna tofauti kubwa sana kati ya shule za serekali na binafisi.
Kama wewe ni msomi kidogo si lazima upeleke watoto
twisheni, unaweza kumfunza mwanao wewe mwenyewe au kumpa ushawishi wa kujiunga kwenye kundi la wale
wanaofaulu vizuri darasani na kusoma pamoja.
Kwa kufanya hivyo utatengeneza fungu ambalo utaweza
kuliwekeza kwenye mifuko ya UTT AMIS au kwingine.
Mbaga anafafanua kuwa, makala hii imejikita sana kwenye
kupunguza anasa (chipsi, kuku na mayai) kama mfano tu, pia imeelezea kirefu jinsi gani mapenzi kwa watotto, wazazi, mke yanaweza kuifanya ndoto yako ififie kwenye uwekezaji.
Najuwa ni vigumu kuwaambia wazazi, pengine hata watoto hapana lakini ili mipango ya pesa iwe ya uhakika inabidi uwe na uwezo wa kukataa jambo fulani ambalo usipolifanya litaleta unafuu katika maisha yako na wao hapo mbele ya safari.
Kumbuka kuwasaidia si kuwapa pesa tu, nenda nao kanisani, mskitini, shamba, wasaidie katika mipango yao, watoto wape maarifa ya masisha wasiwe na akili za darasani tu.
Kwa wazazi tumia mbinu mbalimbali wakuelewe kwani kwa miaka mingi wao walikuwa wameshika usukani sasa unajaribu kuchukuwa nafasi yao, waswahili wanasema mtoto kwa mama hakui.
Kama kuna madeni lazima yalipwe tena kwa mpangilio
maalumu kwani kuwa mwekezaji ukiwa na madeni makubwa tena yenye riba za juu inaweza kuwa tabu sana.
Riba huongeza ukubwa wa deni kama faida jumuishi
inavyokuwa kwenye riba inayoingia kwa mfuko wako.
Tumezungumza kuwa upendo mzuri kwa familia sio chipsi,
mayai na kuku ila kuwekeza ndo upendo wa kweli, uwekezaji utatupa pesa nyingi zaidi na pesa ndiyo kila kitu, wahenga wanasema pesa sabuni ya roho.
Tufanye nini sasa ili twende pamoja katika safari yetu ya
uwekezaji, jambo la kwanza ni kupunguza ugomvi wa hela.
Ni vigumu kukwepa ugomvi wa pesa kati ya mke, mume na
pengine hata ndugu ikiwemo wazazi. Ugomvi wa pesa pengine umefanya hata ndoa au familia kusambaratika.
Bajeti yaweza kuwa vita na hapa ni pale, mahitaji hayawiani na kila mtu anaona hitaji lake ni muhimu zaidi ya mwenzie na pale ambapo kila mtu ana bajeti kivyake.
Kumbuka mkibajeti pamoja ni kama mnawekeza pamoja sababu kila mtu anachangia hivyo fungu la pesa za kutumia pamoja linakuwa kubwa.
Pesa ikiwa nyingi unaweza fanya jambo ambalo awali ulikuwa huwezi kulifanya, miamala inakuwa rahisi na nguvu ya kujadili bei na vitu vingine inaongezeka.
Yabidi kukaa uso kwa uso na kujadiliana tena kiungwana juu ya matumizi yenu kwa pamoja. Mkubaliane tofauti zenu, kumbuka kila binadamu yuko kipekee, hakuna jinsi yeyote ile utakuta watu wawili wanafikiri sawa, na wana tabia sawa.
Hata mapacha hutofautina. Kila mtu aweke shida zake kando na fikra zenu ziende sawa, jaribu kuwa na mtizamo mmoja. Kwepeni kukuza na kuchanganya mambo, viapo kama siwezi thubutu kufanya jambo hilo au kauli kama kila siku unanionea inaleta kinyongo na historia kuwa mwaka jana ulifanya hivi, mwaka huu unarudia tena, ikiwa hivyo hamuwezi kusonga.
Mtofautiane kwa maendeleo, mgombane kwa maendeleo ya kiuchumi na kifamilia. Ugomvi usifute mafanikio au
makubaliano mazuri ya awali.
Kumbukeni pesa ni sabuni ya roho, ugomvi unauma na
unachosha akili. Tunashauriwa kuwa na akaunti za pamoja
lakini kushirikiana kwenye kila senti ni jambo gumu sana kwa wanandoa kwani kila mtu ana matumizi yake binafsi.
Ni vizuri kukubaliana ni kiasi gani kiwekwe pamoja, asilimia ngapi kila mtu abaki nayo kwa ajili ya matumizi binafsi.
Kiasi cha matumizi binafsi ni huru kwa kila mweza kukitumia vile atakavyo bila kuulizwa, hii inatoa uhuru wa kutumia bila uoga kwenye shida au matumizi binafsi.
Kwa mujibu wa Mbaga, usimamizi wa bajeti uwe wa pamoja, hapa haijalishi kama mmoja anafanya kazi na mwingine hafanyi. Ni muhimu kujadili pamoja kipi kifanyike na ni kipi kisifanyike au kisubiri kwanza. Bila kufanya hivyo na kama hakuna uwazi kutoaminiana kutaibuika.
Kumbuka mmekutana ukubwani kila mtu ametoka kwake,
tunaambiwa tusifichine mambo, tusiwe wasiri lakini ikija
kwenye swala la hela inakuwa changamoto kubwa sana.
Cha muhimu ni kupanga pamoja kwa sabubu ugomvi wa pesa na changamoto zake hauishi, kila bili zikija unaibuka, lipa wewe, nimechoka kulipa kila siku.
Kama lengo ni kujenga familia na pesa ndiyo inawatenga ni bora mfikiri mara mbili. Ushauri pangeni pamoja matumizi ya kila siku, fungu la dharura, uwekezaji kwa ajili ya maisha ya mbele.
Haya yawe mambo muhimu katika mpango wenu wa pamoja, kumbuka UTT AMIS ni kampuni ya serekali, njoo tuongee tukatae umaskini, njoo tuwekeze.