Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amewaongoza viongozi na wananchi wa makundi mbali mbali katika zoezi la kupanda miti katika eneo la Shule ya Msingi Dinima Tarafa ya Masanze Januari 27 , 2026.

Tukio hilo adhimu ni sehemu ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alizaliwa tarehe 27 Januari, 1960 katika Kijiji cha Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. 

Katika zoezi hilo wilaya ya Kilosa imekusudia kupanda miti 10,000 katika tarafa saba za wilaya hiyo.