Na. Meleka Kulwa- Fullshangwe Blog, Dodoma
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema kuwa ujenzi wa maabara ya kisasa ya madini katika eneo la Kizota, Dodoma, unatarajia kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya madini nchini, hasa kwa wachimbaji wadogo.
Maabara hio itasadia kuboresha huduma kwa wachimbaji wadogo kwa kuwawezesha kupata taarifa za uchunguzi wa madini yao kwa wakati unaofaa, jambo litakaloongeza tija na ufanisi wa shughuli zao ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto za taarifa zisizo sahihi.
Ameyasema hayo Januari 26,2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kipindi cha siku 100 baada ya Uchaguzi Mkuu.
Mhe. Mavunde amesema kuwa maabara hio kitakuwa na teknolojia ya hali ya juu inayowezesha kuchakata sampuli za madini kwa usahihi mkubwa na kutoa taarifa sahihi na za haraka kwa wachimbaji wadogo pamoja na wadau wa sekta ya madini.
Pia amesema kuwa maabara hicho kitatumika kuhudumia nchi jirani, hivyo kukuza ushirikiano wa kikanda na kukuza biashara za madini katika mkoa wa Afrika Mashariki na Kati.
Aidha, amebainisha kuwa maabara hio itasadia kuboresha huduma kwa wachimbaji wadogo kwa kuwawezesha kupata taarifa za uchunguzi wa madini yao kwa wakati unaofaa, jambo litakaloongeza tija na ufanisi wa shughuli zao ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto za taarifa zisizo sahihi.
Mhe. Mavunde amesema ujenzi wa maabara hio ni sehemu ya jitihada za serikali kuimarisha sekta ya madini kupitia makubaliano na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini ya Finland. ambayo imetuma wataalam wake kuwafundisha wataalamu wa Serikali ya Tanzania (GST) kuendeleza uwezo wa huduma zinazotolewa na maabara hio.
Aidha, amebainisha kuwa Hali hio itahakikisha maabara inakuwa kitovu cha huduma bora kimaabara kusini mwa Jangwa la Sahara.
Aidha, amebainisha kuwa maabara hio itasaidia katika kupanga mikakati ya masoko ya madini ndani na kimataifa, hivyo kuongeza mapato ya taifa na kuinua kipato cha wachimbaji wadogo.
”Hii ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuendeleza sekta ya madini kwa manufaa ya Watanzania wote” amesema waziri Mavunde
Pia, ameeleza kuwa matumizi ya nishati safi ni mojawapo ya mwelekeo muhimu wa serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ni miongoni mwa viongozi vinara wa matumizi ya nishati safi duniani.

