Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikongosi wilaya ya Mufindi
Kabisa wamejipanga kulinda ardhi ya magereza kwa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John
Pombe Magufuli amegiza kuwa magereza yote kuanza kujitegemea kwa kuzalisha
chakula kupitia wafungwa.
wananchi wa kijiji cha Ikongosi wilaya ya Mufindi la kuomba ardhi ya kulima katika
eneo la jeshi la magereza kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi
wakati wa ziara ya Iringa mpya awamu ya pili.
gereza la Isupilo mipaka yake inajulikana na ipo kisheria nay eye hawezi kugawa
eneo hilo hadi pale mamla za juu za serikali zitakavyo amua kwa kuwa kila kitu
kipo kimaandishi.
Iringa Ally Hapi alikataa ombi hilo kwa wananchi wa kijiji cha Ikongosi wakati wa mkutano wa kupokea kero za wananchi
wa wilaya ya Mufindi.
Alisema kuwa ardhi ya magereza ni kwa ajili ya matumizi ya magereza kuzalisha
chakula kwa ajili ya wafungwa.
hata hivyo Hapi alisema kuwa sio kila ombi la wananchi anatakiwa kuwatekelezea
kwani kimsingi ardhi ya magereza ni maalum kwa ajili ya utaratibu wa serikali
kuhifadhi ardhi yake kwa ajili ya matumizi yake ya baadae.
“Serikali ina kawaida ya kuwekeza benki ya Ardhi kwa ajili ya matumizi ya
kijamii ikija kutokea wananchi wameongezeka na serikali inahitaji kujenga kituo
cha afya ama shule benki yake ya ardhi ni kwenye ardhi hiyo iliyowekezwa kwenye
taasisi zake kama magereza,jeshi la kujenga Taifa na maeneo mengine”
Aidha alisema iwapo wananchi wanahitaji eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule
wanaweza kukaa chini na Magereza ili kupewa eneo Ila sio kwa ajili ya kilimo .
Alisema kimsingi shule ni mali ya serikali na magereza ipo chini ya serikali
hivyo wanaweza kupewa eneo la ujenzi na kuwekewa mipaka.
“Ila niwaeleze wazi wananchi kuwa sio kila ombi mnaloomba mnaweza
kusikilizwa maombi mengine hayawezekani kama hili la kuomba ardhi ya magereza
kwa ajili ya kulima watu binafsi”
Hata hivyo Hapi aliagiza magereza kutumia wafungwa kuendeleza ardhi hiyo kwa
kilimo Kama Rais Dkt John Magufuli alivyoagiza kwa magereza zote nchini kutumia
wafungwa kuzalisha chakula Chao wenyewe.