Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi Akizungumza na Wanahabari kuhusu Wajibu wa Wanahabari kuihabarisha jamii juu ya chakula salama, katika Semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kwa Waandishi wa Habari, iliyofanyika Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo Pichani), kuhusu Wajibu wa Wanahabari kuihabarisha jamii juu ya chakula salama katika Semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), kwa Waandishi wa Habari, iliyofanyika Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi(katikati) akitete jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Chakula , Dkt.Kandida Shirima mara baada ya kuzungumza na Waandishi wa Habari katika Semina ya siku mbili iliyoandaliwa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), kwa Waandishi wa Habari , iliyofanyika Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani, kulia ni Afisa Uhusiano(Habari) kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA, Gaudencia Simwanza.
Afisa Mkazi wa PACA (Tanzania), Dkt. Happy Magoha, akijibu swali kutoka kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa PACA juu ya suala la Chakula salama, katika Semina ya siku mbili iliyoandalia na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), kwa Waandishi wa Habari, wiki ya chakula salama iliyofanyika Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Dkt. Analice Kamala, akiwasilisha Mada kwa Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) Kuhusu Athari za Sumu Kuvu kwa Maisha ya binadamu, katika Semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), kwa Waandishi wa Habari , iliyofanyika Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Mataalam wa Masuala ya Chakula Salama kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Roman Fortunatus akijibu swali kutoka kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa Semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kwa Waandishi wa Habari , iliyofanyika Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani.
(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO).
…………………….
Na Paschal Dotto-MAELEZO
Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi amewataka wanahabari kutekeleza majukumu kwa kuihabarisha jamii kuhusu utekelezaji wa utoaji huduma kwa wanajamii ili kuwawezesha kupata uelewa kuhusu mambo Mbalimbali ya Taasisi za Serikali.
Akizungumza katika Semina ya kuwajengea uwezo Wanahabari kuhusu Chakula salama iliyotolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA Wilayani ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Dkt.Abbasi alisema mbali na wajibu wa wanahabari wa Kuburudisha, Kuelimisha na kuhabarisha lakini katika Karne hii ya 21 wanatakiwa kuwa na wajibu wa Aina nyinginezo nne.
Dkt.Abbasi alisema kazi ya kwanza ni kuonyesha changamoto kwenye jamii na kuikosoa Serikali kwa kuibua changamoto zilizoko kwenye jamii ili zipate ufumbuzi na wananchi wapate majibu ambayo yatasaidia kuondokana na changamoto hizo katika maeneo yao
“kukosoa siyo kuandika kwa kuikosoa Serikali tu, bali kama kuna kuna kiwanda kinatiririsha maji machafu, kama kuna sehemu kuna huduma za jamii haziendi sawa, kama kuna Taasisi Binafsi haiendi sawa andika ili kuwasaidia wananchi na jamii kwa ujumla katika maeneo hayo utakuwa umefanya wajibu wako kama mwanahabari”, Dkt. Abbasi.
Dkt.Abbasi alisema Wanahabari watakiwa kuwa na wajibu wa kuhabarisha jamii kuhusu Usalama wa Chakula ili waweze kupata elimu juu ya uandaaji wa chakula salama.
Aidha Dkt.Abbasi alisema kuwa Lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na maisha bora lakini kama lengo halijatimia wanahabari wanawajibu wa kuiambia Serikali kwenye sekta ambazo mambo hayajaenda sawa.
Dkt.Abbasi aliongeza kuwa katika Wajibu mwingine wa wanahabari wanatakiwa kuwa jukwaa la kuwasaidia wananchi kupaza sauti zao katika changamoto mbalimbali, ili kuweza kupata utatuzi wa Changamoto hizo.
“Wajibu Huu unawataka wanahabari, kupata mrejesho Kutoka kwa wananchi wanaonaje kuhusu huduma wanazaopata kutoka kwa Serikali yao, yaani hii inakumbusha kuwa wanahabari wanatakiwa kuwa Jukwaa la maoni ya wananchi na kupaza sauti zao”, alisema Dkt.Abbasi.
Dkt.Abbasi Alisisitiza katika karne ya 21 wanahabari wanatakiwa kuwa na ushirikiano katika kuunga mkono maendeleo ya Jamii, utekelezaji wa Serikali na ahadi zake kwa wananchi, pamoja na kuisifia Serikali pale inapofanya vizuri.
“Kuna wajibu wa Wanahabari kuandika habari juu ya utekelezaji wa maendeleo, sisi kama wanahabari tunawajibu kuwa maendeleo yakitoe unajinasibu nayo, usijitenge na kitu ambacho umekifanya mwenyewe na kikafanikiwa, kama kuna mtaro wa maji machafu wananchi walikuwa wanalalamika, kuna barabara mbovu, kuna huduma za afya zisizoridhisha unaandika kuiambia Serikali, ikitekeleza andika tena kusifu utekelezaji huo” Alisisitiza Dkt. Abbasi.
Pia Dkt.Abbasi aliwataka Wanahabari nchini kushika kanuni hizo mpya kwani ndiyo zitawaongoza Waandishi wa Habari katika Karne hii ya 21.