Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wabunge pamoja na viongozi mbalimbali kabla ya kufungua rasmi Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa na ule wa Afrika Mashariki ukiimbwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.
…………..
Na Meleka Kulwa – Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuanzisha Wizara kamili itakayoshughulikia masuala ya vijana. Amesema hayo leo, tarehe 14 Novemba 2025, wakati akilihutubia Bunge la 13 jijini Dodoma na kuelezea mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita katika mhula wa pili.
Dkt. Samia amesema pia atahakikisha kunakuwepo na Washauri Maalum wa Rais kuhusu masuala ya vijana. “Katika kuhakikisha tunaondoa changamoto za vijana, dhamira yangu ni kuhakikisha tunaanzisha Wizara rasmi inayoshughulikia masuala ya vijana,” amesema.
Amesema pia dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Bima ya Afya kwa Wote inamnufaisha kila Mtanzania. “Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha tunatekeleza Bima ya Afya kwa Wote na kuhakikisha kila Mtanzania anapata matibabu bila changamoto yoyote,” amesema. Dkt. Samia ametoa wito kwa Watanzania kuchangamkia Bima ya Afya kwa Wote ili kupata matibabu bila vikwazo, hata kama hawana fedha pindi wanapoumwa.
Aidha, Serikali itajenga Hospitali Maalum ya Magonjwa ya Mlipuko mkoani Kagera. Kuhusu uimarishaji wa miundombinu ya afya, Dkt. Samia amesema ujenzi na uboreshaji wa vituo vya kutolea huduma utaendelea ili kila mwananchi apate huduma karibu na eneo analoishi. “Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha huduma za afya zinakuwa karibu zaidi na wananchi, hivyo tutahakikisha ujenzi wa Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati unaendelea ili kuleta ufanisi wa huduma,” amesema.
Aidha, Rais Samia amebainisha kuwa Serikali ina dhamira ya kuhakikisha hakuna mtu yeyote atakayezuia maiti hospitalini. “Tunaweka utaratibu maalum mtu aruhusiwe kumzika mpendwa wake na si kuzuia maiti, hivyo bora achukue alipe kidogo kidogo,” amesema Dkt. Samia.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia Bungeni Jijini Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania pamoja na Wakuu wa Taasisi za Kimataifa mara baada ya kufungua rasmi Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. George Mcheche Masaju mara baada ya kufungua rasmi Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania pamoja na Wakuu wa Taasisi za Kimataifa mara baada ya kufungua rasmi Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma tarehe 14 Novemba, 2025.



