KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa, Balozi, Dk.Asha-rose Migiro ametembelea, kukagua na kuridhishwa na maandalizi ya shughuli za kufunga kampeni za uchaguzi za mgombea Urais zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2025 katika viwanja vya CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Dk.Asha-rose amekagua uwanja huo Oktoba 27, 2025 akiwa na jopo lake ambapo ameeleza kuridhishwa na maandalizi hayo kwa asilimia 100, huku tayari mgombea Urais Samiia Suluhu Hassan akiwa amewasili Jijini Mwanza kwa ajili ya tukio hilo.

