Mbunge wa jimbo la arumeru john palangyo akikabidhiwa vitenge maalumu kama ishara ya upendo kutoka kwa wananchi wa makiba leo.
Mbunge wa jimbo la arumeru mashariki akifuraia jambo baada ya kuvishwa shuka la kimasai pamoja na kitenge leo na wananchi wa makiba
…………………………………………………………………………………………..
Na Queen Alex Arusha
Mbunge wa jimbo la arumeru mashariki John Palangyo amemfanananisha Raisi Wa jamuhuri ya Muungano John Magufuli na kiongozi wa kiimani “mfalme Daudi” baada ya kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi jambo ambalo linailetea sifa Nchi kwa ujumla
Aidha mambo ambayo yamesababisha Mbunge huyo kumfananisha na Daudi ni pamoja na mradi wa shirika la ndege,mradi wa treni,pamoja na udhibiti wa madini ambayo yanachimbwa kwenye ardhi ya Tanzania
Palangyo aliyasema hayo mapema leo katika kata ya makiba alipokuwa kwenye ziara yake ya jimbo hilo alioifanya kwa malengo ya kukutana na wananchi wa jimbo hilo.
Alisema kuwa Raisi Magufuli amekuwa kiongozi ambaye ni mwema sana na amefanya kwa kutekeleza ahadi na ilani ya chama cha mapinduzi hali ambayo wakati mwingine inaondoa aibu ya nchi
“Tulikuwa tunapata aibu kubwa sana hasa pale tunapoenda kwenye nchi za watu unaona ndege za nchi hizo zikituq lakini sisi hilo halikiwepo tulikuwa na ndege moja tu sasa tuna ndege nane na zote zinaturaisishia kazi kwanini tusimafananishe na Daudi ambaye alisaulika lakini alivyoshika hatamu ya uongozi watu wake walinufaika zaidi ya kawaida” alihoji mbunge huyo
Mradi mwingine aliongelea mbunge huyo ni pamoja na treni ambazo kwa sasa zimeshaanza kufanya kazi na zitaweza kuraisisha kazi na mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo usafirishaji wa mizigo.
“Mimi nawahakikisha kuwa tuna bahati kubwa sana ya kuweza kupata mafanikio huu mradi ni mkubwa sana na itawanufaisha wengi sana tuna haki ya kumshukuru Raisi wetu” aliongeza Palangyo
Mradi mwingine aliongelea ni udhibiti wa utoroshaji wa madini ambapo hapo awali soko kubwa la madini lilikuwa nje ya nchi wakati madini yenyewe yanachimbwa ndani ya nchi
“Tukiangalia kwa mfano tuu hapo jirani mererani sasa hivi kuna ukuta mkubwa sana utoroshaji haupo tena na wachimbaji nao wana nufaika sana tuna haki ya kumpongeza raisi wetu” alifafanua zaidi
Awali kwa upande wa kata hiyo ya makiba na jimbo zima alisema kuwa tayari ameshafanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha serikali kuleta umeme,kuleta pampu ambayo itaweza kufungwa ili wananchi waweze kuondokana na uhaba wa maji,kuboresha sekta ya afya,sekta ya elimu.
Alimalizia kwa kusema kuwa bado mpaka sasa yeye na ofisi yake wana mikakati mizuri ya kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami kwani inaunganisha mkoa wa Arusha na manyara.