Naibu wa Waziri wa Nishati Bi. Subira Mgalu (wa kwanza kulia) pamoja na Bi. Jokate Mwegelo (wa pili kulia) wakisikiliza Maelezo kutoka kwa Msaidizi wa Usajili Mwandamizi kutoka BRELA, Bi. Leticia Zavu (wa tatu kushoto) walipofika katika Banda la BRELA kwenye Tamasha la Mama Lishe festival lililofanyika siku ya jana tarehe 28 Februari 2020, kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Chanzige, Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jaffo (kulia), akisalimiana na Msaidizi wa Usajili Mwandamizi kutoka BRELA, Bi. Leticia Zavu (kushoto) wakati wa utambulisho Tamasha la Mama Lishe festival lililofanyika siku ya jana tarehe 28 Februari 2020, kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Chanzige, Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
**************************
Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewahimiza Mama lishe wa Mkoa wa Pwani kurasimisha biashara zao kwa kuzisajili ili waweze kulinda biashara zao na kupata fursa mbalimbali.
Rai hiyo imetolewa katika Tamasha la Mama Lishe festival lililofanyika siku ya jana tarehe 28 Februari 2020, kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Chanzige, Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani. Akizungumza katika Tamasha hilo Msaidizi wa Usajili Mwandamizi kutoka BRELA, Bi. Leticia Zavu amebainisha kwamba mara baada ya kurasimisha biashara, ni rahisi kupata ushirikiano katika taasisi zingine.
“Unapokua umesajili biashara yako unakua unaaminika kwa sababu unafanya kwa kuzingatia sheria, hivyo hata katika Taasisi za fedha inakua rahisi kukopesheka”, alisema Bi Zavu. Pia BRELA inasajili vikundi vya watu wanaofanya biashara kuanzia mtu mmoja hadi 20, wanaweza kujiunga na kusajili kikundi chao cha kibiashara, kwa gharama ya Sh. 20,000/