Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Ndugu. Paul Makonda, amemnadi Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. ๐—ฆ๐—ฎ๐—บ๐—ถ๐—ฎ ๐—ฆ๐˜‚๐—น๐˜‚๐—ต๐˜‚ ๐—›๐—ฎ๐˜€๐˜€๐—ฎ๐—ป kwa maelfu ya wananchi wa Arusha Mjini mkoani Arusha waliojitokeza katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid leo tarehe 2 Oktoba 2025.

Ndg. Makonda ameeleza kazi kubwa zilizofanywa na Dkt. Samia ndani ya mkoa wa Arusha zilizoacha alama na matokeo chanya kila kona ya Arusha.

Akieleza kazi hizo, Ndg. Makonda amegusia upanuzi wa uwanja wa ndege wa Arusha ambapo amesema hivi sasa ndani ya Arusha zipo ndege ndogo zenye kutoka Arusha kwenda Nairobi ambapo amesema ni dalili njema ya kuendelea kufungua mkoa wa Arusha na imekuwa kwa mara ya kwanza sasa uwanja huu kupokea ndege kutoka nje ya nchi moja kwa moja tofauti na awali ilivyokuwa wakilazimika kwenda viwanja vingine kupata vibali kabla ya kutoa uwanjani hapo.

Ndg. Makonda ameeleza kuwa upanuzi wa uwanja huo ni fursa kwa wafayabiashara na watalii kutoka nje ya nchi kupunguza gharama na kupoteza muda mwingi ambapo amebainisha kuwa ni hatua kubwa ya kukuza uchumi.

Pia, Ndg. Makonda ameeleza kuwa kupitia maelekezo ya Dkt. Samia, mkoa wa Arusha umefanikiwa kutekeleza miradi iliyokwama kwa miaka mingi ambapo amebainisha kuwa zaidi ya bilioni 64 zimetumika na katika jimbo la Arusha mjini tayari ujenzi wa stendi kubwa na ya kisasa ya mkoa imeanza kujengwa pamoja na soko kubwa la kisasa pia linajengwa.

Vilevile, amesema kuwa wananchi wa Arusha wanafurahia uongozi bora wa serikali ya awamu ya sita inayotokana na CCM kwakuwa kulikuwa na changamoto ya umeme lakini sasa umeme wa rea umepatikana na wananchi wanaunganishiwa huduma kwa shilingi 27,000/= tu jambo ambalo limezidi kupania wigo wa upendo wa Watanzania wote kwa CCM.

Aidha, Ndg. Makonda ametoa shukrani zake za kipkee kwa Mgombea Urais Dkt. Samia kwa kuendelea kumuamini na kuamini katika vijana.

“..๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฑ๐˜ฆ๐˜ฌ๐˜ฆ๐˜ฆ ๐˜ฏ๐˜ช๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ด๐˜ฉ๐˜ถ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ณ๐˜ถ ๐˜ฌ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ฏ๐˜บ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ข๐˜ต๐˜ช ๐˜ป๐˜ฐ๐˜ต๐˜ฆ ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ฏ๐˜ช๐˜ข๐˜ฎ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช ๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ฏ๐˜ช๐˜ฑ๐˜ข ๐˜ฉ๐˜ฆ๐˜ด๐˜ฉ๐˜ช๐˜ฎ๐˜ขย ๐˜ฌ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ฏ๐˜ข๐˜ง๐˜ข๐˜ด๐˜ช ๐˜ป๐˜ข ๐˜ถ๐˜ต๐˜ถ๐˜ฎ๐˜ช๐˜ด๐˜ฉ๐˜ช ๐˜ฌ๐˜ข๐˜ฎ๐˜ข ๐˜”๐˜ธ๐˜ฆ๐˜ฏ๐˜ฆ๐˜ป๐˜ช ๐˜ธ๐˜ข ๐˜Š๐˜Š๐˜”, ๐˜ฎ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ถ ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ฌ๐˜ฐ๐˜ข ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ˆ๐˜ณ๐˜ถ๐˜ด๐˜ฉ๐˜ข ๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ฉ๐˜ข๐˜ต๐˜ช๐˜ฎ๐˜ข๐˜บ๐˜ฆ ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ฑ๐˜ช๐˜ต๐˜ช๐˜ข ๐˜ท๐˜ช๐˜ฌ๐˜ข๐˜ฐ ๐˜ท๐˜ช๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ฃ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ท๐˜บ๐˜ข ๐˜ค๐˜ฉ๐˜ข๐˜ฎ๐˜ข ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ฏ๐˜ช๐˜ณ๐˜ฆ๐˜ซ๐˜ฆ๐˜ด๐˜ฉ๐˜ข ๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ฃ๐˜ข๐˜ข๐˜ฅ๐˜ข๐˜บ๐˜ฆ ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ด๐˜ฉ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ฅ๐˜ข ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ณ๐˜ข ๐˜ป๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ข๐˜ฐ๐˜ฏ๐˜ช ๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ณ๐˜ฆ๐˜ซ๐˜ฆ๐˜ด๐˜ฉ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ต๐˜ฆ๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜จ๐˜ฐ๐˜ฎ๐˜ฃ๐˜ฆ๐˜ข ๐˜ถ๐˜ฃ๐˜ถ๐˜ฏ๐˜จ๐˜ฆ ๐˜ฌ๐˜ข๐˜ต๐˜ช๐˜ฌ๐˜ข ๐˜ซ๐˜ช๐˜ฎ๐˜ฃ๐˜ฐ ๐˜ญ๐˜ข ๐˜ˆ๐˜ณ๐˜ถ๐˜ด๐˜ฉ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ซ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช..”

“..๐˜‹๐˜ฌ๐˜ต. ๐˜š๐˜ข๐˜ฎ๐˜ช๐˜ข ๐˜ธ๐˜ฆ๐˜ธ๐˜ฆ ๐˜ฏ๐˜ช ๐˜”๐˜ข๐˜ฎ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ธ๐˜ฆ๐˜ฎ๐˜ข ๐˜ด๐˜ข๐˜ฃ๐˜ข, ๐˜ด๐˜ช ๐˜ฌ๐˜ธ๐˜ข๐˜ฃ๐˜ข ๐˜ถ๐˜ฎ๐˜ฆ๐˜ด๐˜ช๐˜ฎ๐˜ข๐˜ฎ๐˜ช๐˜ข ๐˜ท๐˜ช๐˜ฌ๐˜ข๐˜ฐ ๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ฏ๐˜ช๐˜ต๐˜ฆ๐˜ถ๐˜ข ๐˜ฌ๐˜ธ๐˜ฆ๐˜ฏ๐˜บ๐˜ฆ ๐˜ฏ๐˜ข๐˜ง๐˜ข๐˜ด๐˜ช ๐˜ฎ๐˜ฃ๐˜ข๐˜ญ๐˜ช๐˜ฎ๐˜ฃ๐˜ข๐˜ญ๐˜ช ๐˜ญ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช ๐˜ฃ๐˜ข๐˜ฅ๐˜ฐ ๐˜ถ๐˜ฎ๐˜ฆ๐˜ฆ๐˜ฏ๐˜ฅ๐˜ฆ๐˜ญ๐˜ฆ๐˜ข ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ต๐˜ถ๐˜ญ๐˜ฆ๐˜ข ๐˜ท๐˜ช๐˜ซ๐˜ข๐˜ฏ๐˜ข, ๐˜”๐˜ถ๐˜ฏ๐˜จ๐˜ถ ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ฃ๐˜ช๐˜ฏ๐˜จ๐˜ถ๐˜ฏ๐˜ช ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ต๐˜ถ๐˜ฏ๐˜ป๐˜ฆ ๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ญ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ฅ๐˜ข..”