Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asharose Migiro amewasili na kupokelewa na maelfu ya wananchi wa Moshi mkoani Kilimanjaro katika viwanja vya mashujaa leo tarehe 1 Oktoba 2025.

Dkt. Migiro ametoa salamu za upendo kutoka kwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. ๐—ฆ๐—ฎ๐—บ๐—ถ๐—ฎ ๐—ฆ๐˜‚๐—น๐˜‚๐—ต๐˜‚ ๐—›๐—ฎ๐˜€๐˜€๐—ฎ๐—ป kwa wananchi hao huku akiwaeleza kuwa ujio wa Dkt. Samia ni kwaajili ya kuomba kura ili kuendelea kufanya yale yote mazuri aliyoyafanya katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.

Wananchi hao pia wameonesha utayari na kumthibitishia Dkt. Migiro kuwa wapo sambamba na CCM na watakipigia kura nyingi ifikapo Oktoba 29 katika uchaguzi mkuu.

Dkt. Samia atakuwa hapa kuendelea na mikutano yake ya kampeni za Urais katika kunadi Ilani, Sera na Ahadi za CCM.