NA JOHN BUKUKU – MOSHI
Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anatarajiwa kuendelea na mikutano ya kampeni leo, Jumatano Oktoba 1, 2025, katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, ambapo atahutubia maelfu ya wananchi katika maeneo ya Moshi Mjini, Bomang’ombe na Usa River.
Katika mkutano wa Moshi Mjini, mgombea huyo ataeleza mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa CCM na kueleza dhamira ya serikali ijayo kuendeleza miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara. Wananchi wa Moshi wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kumsikiliza kutokana na historia ya chama hicho katika mkoa huo.
Baada ya Moshi, msafara wa kampeni utahamia Bomang’ombe wilayani Hai, ambapo mgombea atakutana na wananchi na kuwaeleza mikakati ya serikali ya kuimarisha kilimo na biashara ndogondogo, sambamba na kuhimiza mshikamano wa vijana katika kushiriki shughuli za maendeleo.
Jioni ya leo, mgombea ataendelea na mkutano mkubwa Usa River mkoani Arusha. Huu ni mkutano muhimu kwa kuwa Arusha ni lango la biashara na utalii nchini, hivyo hotuba ya mgombea inatarajiwa kuangazia miradi mikubwa ya kiuchumi, uwekezaji katika sekta ya utalii na nafasi za ajira kwa vijana.
Wananchi wa Kilimanjaro na Arusha wanahimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mikutano hiyo ili kusikiliza sera na mipango ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani oktoba 29,2025
