Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM akizungumza na mtoto Mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 30 Septemba, 2025.
………..
NA JOHN BUKUKU- MWANGA KILIMANJARO
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wakulima wa Wilaya ya Mwanga kwa juhudi zao katika kilimo na kuahidi kuwajengea soko jipya kubwa litakalosaidia kuboresha biashara na kuongeza kipato chao.
Akizungumza na wananchi wa Mwanga Septemba 30, 2025, wakati wa kampeni zake za uchaguzi, Dkt. Samia alisema wakulima wa eneo hilo wameonyesha kuwa ni miongoni mwa wazalishaji bora na kwamba serikali ya CCM imejipanga kuboresha mazingira ya masoko ili mazao yao yaweze kuwanufaisha zaidi kiuchumi.
“Niwapongeze Wana Mwanga maana ni wakulima wazuri,” alisema Dkt. Samia, akibainisha kuwa soko kubwa litajengwa katika eneo la Chita kwa lengo la kuongeza thamani ya mazao na kuimarisha biashara ya wakulima.
Aidha, alieleza kuwa soko jipya litakuwa la kisasa na kituo kikuu cha biashara ya mazao, jambo litakalorahisisha wakulima kupata masoko ya uhakika na bei nzuri zaidi. Hata hivyo, hakutaja gharama za ujenzi wa soko hilo, akibainisha kuwa maelezo ya kifedha na utekelezaji wake yatatolewa na Serikali kupitia wizara na halmashauri husika.
Kwa sasa, Wilaya ya Mwanga imekuwa ikitegemea masoko madogo ya kijamii na ya mitaa ambayo hayana uwezo mkubwa wa kuhudumia wakulima wote. Ujenzi wa soko jipya Chita unatarajiwa kuondoa changamoto hiyo na kuchochea maendeleo ya kiuchumi ya wananchi wa Mwanga.
Aidha, alisema serikali itaendelea kuboresha huduma za kijamii na miundombinu katika Wilaya hiyo, ikiwemo kuongeza minara ya mawasiliano, kuboresha sekta ya utali.
