Mkuu wa Mahusiano ya Biashara wa Benki ya Equity, Eric Shao (katikati) akimkabidhi hati za makubaliano Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Kashilimu Mayunga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mzunguko wa Makole (Round About) na kuanzisha rasmi utaratibu wa kuwakopesha wananchi wanaohitaji huduma ya Maunganisho mapya ya Maji safi na Maji taka. Hafla hiyo ilifanyika katika mzunguko huo wa Makole jijini Dododma leo. Kulia ni Naibu Meya wa jiji la Dodoma, Emmanuel Chibago akishuhudia. (Picha Zote na Muhidin Sufiani).
Mkuu wa Mahusiano ya Biashara wa Benki ya Equity, Eric Shao (wa pili kulia) akimkabidhi hati za makubaliano Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Kashilimu Mayunga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mzunguko wa Makole (Round About) na kuanzisha rasmi utaratibu wa kuwakopesha wananchi wanaohitaji huduma ya Maunganisho mapya ya Maji safi na Maji taka. Hafla hiyo ilifanyika katika mzunguko huo wa Makole jijini Dododma leo. Katikati yao ni Naibu Meya wa jiji la Dodoma, Emmanuel Chibago (kulia) ni mwakilishi wa Water.org, Emmanuel Kanagisa.
Meya akitazama mandhari ya bustani ya Mzunguko huo baada ya uzinduzi.
MAFUNZO MAALUM
MENEJA Mradi Wash kutoka Benki ya Equity, Johanes Msuya, akizungumza wakati akifafanua baadhi ya vigezo vya mwananchia anayetakiwa kupewa mkopo wa kufungiwa vifaa vya maji safi na maji taka wakati wa mafunzo maalumu yaliyofanyika katika ukumi wa Royal Village baad aya uzinduzi wa Mzunguko wa Makole (Round About) na kuanzisha rasmi utaratibu wa kuwakopesha wananchi wanaohitaji huduma ya Maunganisho mapya ya Maji safi na Maji taka. Hafla hiyo ilifanyika katika mzunguko huo wa Makole jijini Dododma leo.
Mkuu wa Mahusiano ya Biashara wa Benki ya Equity, Eric Shao, akifafanua jambo katika mafunzo hayo.
Naibu Meya wa Jiji la Dodoma, akiuliza swali kwa niaba ya wananchi walengwa wa mkopo huo.
Meneja Msimamizi na muangalizi wa Kitengo cha Mikopo Benki ya Equity, Joseph Samson, akifafanua jambo.
Naibu Meya wa jiji la Dodoma, Emmanuel Chibago, akibofya kitufye kuashiria kuzindua rasmi wa Mzunguko wa Makole (Round About) na kuanzisha rasmi utaratibu wa kuwakopesha wananchi wanaohitaji huduma ya Maunganisho mapya ya Maji safi na Maji taka. Hafla hiyo ilifanyika katika mzunguko huo wa Makole jijini Dododma.
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) kwa kushirikiana na Benki ya Equity wameandaa utaratibu wa kukopesha fedha kwa watu wa hali ya chini ili waweze kuunganishiwa maji.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Mkuu wa Biashara wa Benki ya Equity Erick shayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo.
Shayo alisema kwa kupitia utaratibu huo watu wenye kipato cha chini wataweza kupewa mikopo ili waweze kuunganishia maji na kisha kuresha mkopo huo taratibu.
Alisema,mikopo hiyo itawawezesha kila mkazi wa Dodoma ambaye hana kipato kuweza kuwa na huduma hiyo kwani ni muhimu katika kulinda afya.
“Dodoma hivi sasa ni Jiji hivyo ni lazima kila mmoja awe na huduma maji, Nasisi tumejipanga ili kuweza kuwafikia hata watu wa vijijini wenye kipato cha chini kuweza kunufaika na Benki yao” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Kashilimu Mayunga, akizungumza jambo wakati wa uzinduzi huo.
Naibu Meya wa jiji la Dodoma, Emmanuel Chibago, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mzunguko wa Makole (Round About) na kuanzisha rasmi utaratibu wa kuwakopesha wananchi wanaohitaji huduma ya Maunganisho mapya ya Maji safi na Maji taka. Hafla hiyo ilifanyika katika mzunguko huo wa Makole jijini Dododma.
******************************************************************
Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Emmanuel Chibago, alisema utaratibu wa Benki hiyo ni mzuri kwani unawezesha watu wa ngazi hiyo nao kupata huduma hiyo.
Chibago alisema ni vyema mikopo hiyo ikawafikia hata watu wa vijijini na isiwe yenye riba kubwa kwani uwezo wa wananchi hao ni mdogo.
“ Tunaomba utaratibu huu usiwe kwa Benki ya Equity peke yake bali na taasisi zingine za fedha kuiga utaratibu huu” alisema.
Naye Johanes Msuya, ambaye ni meneja wa miradi wa Benki ya Equity alisema mradi wa kutoa mikopo hiyo haitaishia Dodoma tu bali utaenda katika mikoa nane hapa nchini.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dodoma, Dar-es-Salaam,Mwanaza, Mbeya, Iringa, Arusha, Morogoro, na Kilimanjaro.
Kwa upande wake Emmanuel Kangisa ambaye ni mwakilishi wa kampuni ya “Water.Org”, alisema wao watahakikisha wanatunza vyanzo vya maji ili kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana kwa uhakika.
Alisema kampuni hiyo inafanya kazi kwa pamoja na benki ya Equity ili kufanikisha upatikanaji wa maji hayo kwa kaya zenye kipato cha chini.
“ Na hata hizi fedha zitakapo kopeshwa zikifika kwenye akaunti ya walengwa zitaenda moja kwa moja DUWASA ili kuthibiti matumizi ambayo hayakulengwa na benki hiyo’ alisema.
Awali kizungumza katika uzinduzi wa mzunguko wa barabara ya makole Jijini hapa,
Naibu Meya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi.
Naibu Meya akipiga bpicha na Mhandisi aliyejenga mzunguko huo wa Makole.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi.