Mwenyekiti wa kikao cha bunge la EALA Nzeintin Nahimana akiingia kuongoza kikao cha Tatu cha bunge la Nne jioni hii jijini Arusha
Mwenyekiti wa kikao cha tatu Nzelentin Nahimana akiwa kwenye chumba baada ya kupitishwa kuwa Mwenyekiti wa kikao cha bunge la nne kuongoza kikao cha Tatu cha bunge hilo leo jioni jijini Arusha. |
Ahmed Mahmoud Arusha
Bunge la Afrika mashariki limempitisha Mbunge wa bunge hilo Leontin Nzeimanah kuwa Mwenyekiti wa Kikao cha Tatu mkutano wa nne kuendesha baada ya Spika kutotokea kwenye kikao hicho.
Bunge hilo liliingia kwenye mjadala wa muda na hatimaye kufikia muafaka wa kumchagua Mwenyekiti wa Kikao ili kuendelea na shughuli za bunge hilo baada ya Spika kutotokea kwa sababu za kibinadamu jambo ambalo sheria inaweka wazi kupatikana kwa Mwenyekiti wa kuendesha kikao hicho.
Mh.Nzelentin Nahimana mbunge kutoka nchini Burundi alipigiwa kura 27 dhidi ya Mbunge Fatuma Ndangiza aliepata kura 18 ambapo jumla ya kura zilizopigwa ni 45 Kwa wajumbe wote 54 wa bunge hilo.
Akiongea na vyombo vya habari Mara baada ya kutoa hoja ya kumchagua Mwenyekiti huyo Mbunge wa bunge hilo Abdulkadir Aden alitoa hoja kwa baraza hilo kuona umuhimu wa kuwa na Naibu Spika ili siku ambayo Spika hayupo shughuli ziweze kuendelea.
“Naomba baraza la mawaziri kuona umuhimu wa kulipeleka suala hili kwa mkutano wa Marais kuona linafanyiwa kazi na kuondoa changamoto hii ambayo imekuwa ikitokea kila wakati.
Kwa upande wake Mbunge wa bunge hilo Mhandisi Habib Mnyaa alisema haoni sababu ya kuwepo kwa Spika na Naibu Spika wakati sheria ipo ya kuchagua Mwenyekiti wa kuendesha kikao pindi Spika akiwa hayupo kwa sababu za kibinadamu.
Alisema kuwa bunge hilo bado ni dogo halina bajeti yenye kukidhi matakwa hayo na gharama ni kubwa za kumlipa Naibu Spika haoni sababu kuwa ni kiti hicho kwa Sasa Ila sekretariet ikiona inauwezo wa kifedha hakuna shida.
“Jua kuwa sheria zipo za kuendesha bunge hili jumuiya hii bado ni ndogo mimi sioni sababu ya kuwa na Naibu Spika kwa Sasa ikiwa ni kupunguza gharama na bado sheria zipo hivyo busara ipo mikononi mwa wakuu wa nchi kubadilisha sheria”