Katibu
wa CCM Mkoa wa Simiyu, Haula Kachwamba akibeba samaki aina ya sangara mwenye
urefu wa sentimita 90 akiwa na uzito wa kilo
15 baada ya kutembelea Mwalo wa Nyamikoma Busega Simiyu na kushangazwa na mafanikio ya Serikali ya kudhibiti uvuvi haramu
KATIBU
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Haula Kachwamba akikagua zana
haramu zilizokamatwa katika Mwalo wa Nyamikoma wilayani Busega mkoani Simiyu
wakati wa ziara ya Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Mkoa Simiyu kukagua
utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye Sekta ya Uvuvi. Kulia ni Afisa Mfawidhi Ulinzi
na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kanda ya Simiyu na Magu, Samson Mboje.

Na Mwandishi Wetu, Simiyu
CHAMA cha Mapinduzi kimeshtushwa na ongezeko kubwa la samaki
aina ya Sangara ikiwa ni miaka mitatu tu tangu Serikali ya awamu ya tano kuanza
operesheni za kudhibiti uvuvi haramu katika Ziwa Victoria na kutaka Serikali
kuchukua hatua za haraka kutafuta masoko ya uhakika ya samaki ndani na nje ya
nchi.

Wakizungumza kwenye ziara ya Wajumbe wa Sektetarieti ya
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu baadhi ya Wavuvi katika Mwalo wa Nyamikoma
wilayani Busega wamesema awali kabla ya operesheni kuanza walikuwa
wakisafirisha wastani wa tani 6 za samaki kwa mwezi lakini tangu Serikali
ilipoamua kuchukua hatua za kudhibiti uvuvi haramu samaki wameongezeka na sasa
wanasafirisha wastani wa tani 60 kwa mwezi.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi ‘BMU’
Mwalo wa Nyamikoma wilayani Busega mkoani Simiyu , George James alisema
ongezeko hilo kubwa la samaki pia limepunguza bei ya Sangara kutoka wastani wa
shilingi 9,000 kwa kilo hadi kufikia
shilingi 4,000 kwa kilo.

Mbali na mafanikio hayo pia wavuvi hao wameiomba Serikali
kuwasaidia kupata mtambo wa kutengeneza barafu katika eneo hilo kwani kwa sasa
wanalazimika kusafiri hadi jijini Mwanza umbali wa zaidi ya kilomita 150
kufuata barafu.

Hivyo walimuomba Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu kumfikishia
shukrani Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa uongozi wake imara hasa katika usimamizi
wake wa rasilimali za uvuvi na kwamba sasa samaki ni wengi na kwamba ombi lao
kubwa ni kusaidiwa kupata soko baada ya ongezeko hilo la samaki.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Mwalo wa Nyamikoma wilayani Busega, Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Haula
Kachwamba aliitaka Serikali kupitia
Dawati la Sekta Binafsi lililoko Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufika katika mwalo
huo wa Nyamikoma ili kuwaunganisha wavuvi hao na taasisi za kifedha kuweza
kupata mtambo wa kutengeza barafu.

Pia ameitaka Serikali kutanua wigo wa kuwatafutia masoko ya
samaki wavuvi hao ili kunufaika na fursa kubwa ya ongezeko hilo la samaki aina
ya Sangara kwa kupeleka katika masoko ya mikoa ya mbali na Ziwa Victoria pamoja
na nchi za jirani za Kongo, Zambia, Burundi, Rwanda, Malawi na Msumbiji.

Kuhusu vita dhidi ya uvuvi haramu, Katibu huyo alisema Ilani
ya CCM imeitaka Serikali kudhibiti uvuvi ili kupata uvuvi endelevu na kuongeza
kipato cha mwanchi mmoja mmoja na kuiletea fedha za kigeni Serikali kutokana na
mauzo ya samaki nje ya nchi na kupongeza juhudi kubwa zilizofanywa na Rais Dk.
John Magufuli katika kusimamia rasilimali hizo za uvuvi.

“Tunaishukuru Serikali kwa kuamua na kusimamia operesheni
Sangara ambayo ilisimamiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi operesheni hii imezaa
matunda kama mlivyotoa ushuhuda kwamba operesheni hii mliipinga sana lakini
sasa mnaona matokeo yake”alisema.

Aliongeza kuwa CCM inaamini katika kusimamia sheria na
kwamba hatua zote zilizochukuliwa na Serikali katika kudhibiti uvuvi haramu
zililenga kunufaisha watanzania wengi tofauti na hapo awali ambapo watu
wachache ndio waliokuwa wakinufaika kupitia uvuvi haramu.

“Niipongeze sana Serikali yetu kwa kukubali kutukanwa,
kuzuliwa maneno mengi kupata kashfa nyingi lakini bado waliendelea kusimamia
msimamo wa kulinusuru ziwa letu kwenye ilani yetu tumesema tutahakikisha
tunadhibiti uvuvi haramu ili tuweze kupata samaki wa kutosha kwa ajili ya
watanzania sisi CCM tunaomba msiishie hapa endeleeni kudhibiti uvuvi haramu ili
matunda yazidi kuongezeka siku hadi siku”alisema Katibu wa CCM

Katika hatua nyingine, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya
Busega, David Palanjo aliongoza zoezi la uteketekezaji wa shehena ya nyavu
haramu zilizokamatwa kwenye operesheni hiyo katika wilaya za Magu na Busega na
kutoa wito kwa wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kudhibiti uvuvi
haramu.