Mgombea ubunge wa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro Kupitia Chama Cha Ukombozi wa umma (CHAUMA) james Mbowe amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa na tume huru ya Taifa ya uchanguzi (INEC) ili kuwania nafasi ya ubunge Katika uchaguzi Mkuu ujao.
Mbowe amekabidhiwa Fomu hiyo Leo, jumanne Agost 26,2025 na msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Hai,Aidan Angetile Makalata Katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo Hilo.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Makalata amesema nyaraka zilizowasilishwa na james Mbowe kugombea nafasi hiyo zimekidhi vigezo vilivyowekwa na kumtaka kuhakikisha anarejesha Fomu hizo ndani ya muda uliyopangwa kabla ya Siku ya uteuzi.
