Dar es Salaam, 25 Agosti 2025
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Ndg. Luhaga Joelson Mpina, jana aliwasili katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kisheria zinazohitajika kabla ya kuanza rasmi kampeni za uchaguzi mkuu.
Mpina aliambatana na Mgombea Mwenza wake, Bi. Fatma Fereji, ambapo kwa pamoja walikula kiapo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Ndg. Hussein S. Mtembwa.
Taratibu hizo ni sehemu ya masharti ya kisheria yanayowataka wagombea wote wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutimiza wajibu huo kabla ya kuanza kwa mikutano ya kampeni.
Kwa hatua hiyo, wagombea hao wa ACT-Wazalendo sasa wako tayari kuingia katika hatua inayofuata ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

