Na Mwandishi Wetu – Igunga, Tabora

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Ndugu Luhaga Mpina, leo Agosti 22, 2025 amefika wilayani Igunga mkoani Tabora kwa madhumuni ya kuomba udhamini ili kukidhi vigezo vya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kugombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Ziara hiyo ni sehemu ya mchakato rasmi unaoendelea wa wagombea wa nafasi ya Urais kuhakikisha wanatimiza masharti ya kisheria ikiwemo kupata idadi ya wadhamini wanaohitajika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.

ACT-Wazalendo kupitia kaulimbiu yake ya Linda Kura imekuwa ikisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kisiasa na kulinda haki yao ya kidemokrasia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.