NA DENIS MLOWE IRINGA
MAELFU ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa wamejitokeza kwa wingi kuwa wadhamini wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM Dk. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Wanachama hao wakiongozwa na viongozi mbalimbali wa Chama na watia nia mbalimbali walijitokeza katika ukumbi wa ofisi za CCM mkoa akiwemo mwenezi wa Ccm wilaya ya Mufindi, Dickson Lutevele , mkuu wa wilaya ya Mufindi, Dk. Linda Salekwa , Mchungaji Peter Msigwa watia nia udiwani ikiwemo Sara Ponela.
Akizungumza mara baada ya kumdhamini Rais , Lutevele alisema kuwa kujitokeza kwa wingi kwa wananchama kutokana na imani kubwa juu ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo kwa vitendo.
Alisema pamoja na muda mfupi wa maandalizi, muitikio wa wananchi ulikuwa mkubwa kutoka makundi mbalimbali yakiwemo waendesha bodaboda, wazee wa mila na vikundi vya kijamii ambao ni wanachama kujitokeza mkoa mzima.
Dickson Lutevele alisema kuwa wana Iringa wamepanga kumpa kura za kishindo Mama Samia na wamejipanga vyema kuibuka na kura za kutosha kwa ajili ya rais.
Naye aliyekuwa mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Ritah Kabati alisema kuwa kujitokeza kwa wingi wanachama kumdhamini Rais Samia ni ishara tosha ya kukubalika kwa chama na kama mwanamke inaonyesha ni kiasi gani kazi ya kuleta mabadiliko imefanyika
Alisema kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo imeletwa chini ya mwanamama shupavu hali ambayo imeanza kujionyesha mapema kutokana n umati wa wanachama walivyojitokeza.
Kwa upande wake Sara Ponela alisema kuwa tngu asubuhi tumeona makundi mbalimbali ya watu ambao ni wanachama, wafanyabiashara , Bodaboda na makundi ya jamii wakiwa wamekuja hapa kwa lengo la kumdhamini mgombea wetu licha ya kwamba utaratibu ulihitaji wanachama 200 ila hapa kuna wanachama zaidi ya 4000 wamejitokeza.
Nina furaha sana kumdhamini mh Rais kwani mambo aliyofanya nchini ni makubwa hivyo mitano tena.




