Na Hellen Mtereko,Mwanza
Mkurugenzi wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), David Kafulila ameeleza namna ambavyo diplomasia ya kiuchumi ikizingatiwa inavyoweza kuchochea maendeleo ya nchi nakusaidia kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050.
Amesema Diplomasia ya kiuchumi ni msingi mkubwa sana usioonekana lakini unamatokeo makubwa sana na kila walipokosea kwenye eneo hilo palikuwa na athali kubwa kwenye uchumi.
Aidha, alieleza kuwa nchi ikiwekeza katika rasilimali watu,nafasi ya kijiografia na diplomasia ya kiuchumi itaweza kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya 2050.
“Kwa mfano Serikali ya awamu ya sita baada ya kufungua uchumi na kuboresha diplomasia yake katika uchumi,biashara ya Tanzania duniani imeongezeka ambapo Kwa mwaka 2021 mauzo na manunuzi ya nje yalikuwa takribani Dola milioni 17 lakini Sasa ni zaidi ya sola milioni 34 hii ni kwasababu ya kufanya juhudi kubwa katika kuijenga diplomasia ya kiuchumi”, amesema Kafulila
Amesema nafasi ya jiografia ya Tanzania ikibadilishwa kiuchumi inaweza kuchangia kuliko sekta yoyote Ile, hii ni kutokana na kupakana na mataifa mengi yasiyo na bandari.