Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga, akizungumza wakati akihitimisha wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa yaliyofanyika katika ukumbi wa Mabele uliopo Mabeyo Complex, Jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga,(hayupo pichani) wakati akihitimisha wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa yaliyofanyika katika ukumbi wa Mabele uliopo Mabeyo Complex, Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Suleiman Mvunye, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa yaliyofanyika katika ukumbi wa Mabele uliopo Mabeyo Complex, Jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Vijana, Bw. Arafat Lesheve, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa yaliyofanyika katika ukumbi wa Mabele uliopo Mabeyo Complex, Jijini Dodoma.
Na.Mwandishi Wetu-DODOMA
SERIKALI imesema itaendelea kuongeza fursa za ajira kwa vijana nchini pamoja na kuweka mazingira wezeshi yatakayowawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Ummy Nderiananga, wakati akihitimisha wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa yaliyofanyika katika ukumbi wa Mabele uliopo Mabeyo Complex, Jijini Dodoma.
“Vijana ni nguzo muhimu ya maendeleo ya taifa. Serikali itaendelea kushirikiana nao na kuhakikisha kuwa inawawekea mazingira rafiki ya kuwawezesha kujiajiri na kuajiriwa,” amesema Mhe. Nderiananga.
Amebainisha kuwa asilimia 34.5 ya Watanzania ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35, hivyo Serikali imejipanga kuhakikisha kundi hilo linawezeshwa ipasavyo ili kufikia malengo yao.
Aidha, ameeleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inaratibu programu mbalimbali za vijana zinazotekelezwa na Wizara nyingine katika sekta mbalimbali, ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, mikopo ya asilimia 10 kutoka halmashauri pamoja na mifuko mingine ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
“Lengo letu ni kuhakikisha vijana wananufaika na mikopo himilivu itakayowawezesha kuanzisha miradi ya kujiajiri na pia kuajiri wenzao,” amefafanua
Kwa upande wa kukuza ujuzi, Mhe. Nderiananga amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi kwa Vijana, kupitia mafunzo ya ufundi stadi, ujasiriamali na stadi za kazi yanayotolewa katika vyuo vya ufundi vilivyopo nchini.
Aidha, amesema kuwa Serikali imepanga kuanzisha Kituo Maalum cha Maendeleo ya Ujuzi kwa Ajira za Nje ya Nchi (Skills Development Center for Overseas Employment), ambacho kitasaidia kuwaandaa vijana wa Kitanzania kuhimili ushindani wa soko la ajira kimataifa.
Pamoja na hayo, amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha vijana wanapata nafasi na nyenzo za kufikia mafanikio yao binafsi na ya kitaifa.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Dkt. Majaliwa Marwa amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na asasi za vijana katika kukuza ujuzi wa kidijitali kupitia vituo vya ubunifu, kuimarisha afya ya uzazi kwa vijana, kuongeza ushiriki wao katika ujenzi wa amani, majadiliano ya kijamii, na mifumo ya uwajibikaji ili kuhakikisha hakuna kijana anayesahaulika.
Naye, Mwakilishi wa Vijana, Bw. Arafat Lesheve ametoa wito kwa Serikali, sekta binafsi, mashirika ya kiraia na jamii kwa ujumla kuendelea kuwawezesha vijana na kuwashirikisha kikamilifu katika kila hatua ya maendeleo ya taifa, hususan kuelekea Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.