Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan
Zungu akiongea na wawekezaji wa Nishati ya kupikia aina ya gesi kutoka Kampuni
ya KOPAGas. Kampuni hiyo imelenga kusambaza nishati ya gesi majumbani kwa
gharama nafuu kwa mfumo wa ‘kulipia kadiri ya unavyotumia’ Wawekezaji hao
wamemtembelea Waziri Zungu katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais, Mtaa wa
Luthuli jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan
Zungu hii leo ameungana na kikundi cha Pamoja Youth katika zoezi la Upandaji miti
katika Shule ya Sekondari Buguruni-Moto. Takriban miti 100 imependwa katika eneo
hilo ikiwemo miti ya matunda na miti ya vivuli.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan
Zungu akiongea na Bw. Stanslav Toldy raia wa Uingereza akiwa ni sehemu ya
wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika uzalishaji wa magari yenye kutumia nishati
ya umeme. Wawekezaji hao wamemtembelea Waziri Zungu katika Ofisi ndogo ya
Makamu wa Rais, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.