****************************
Ushiriki wa Tanzania kwenye Maonesho ya Dunia (EXPO 2020). Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa nchi zaidi ya 192 zinazotarajiwa kushiriki Maonesho ya Dunia (Expo 2020 Dubai) yanayotarajiwa kufanyika mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuanzia mwezi Oktoba 2020 hadi Aprili 2021 (miezi
6).
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki wanaratibu ushiriki wa Maonesho haya.
Maonesho haya hufanyika kila baada ya miaka mitano (5) yakiwa na lengo mahususi katika kukuza mahusiano ya
kiuchumi, uwekezaji, kidplomasia na kijamii baina ya nchi.
Lengo la Maonesho ya Expo 2020 Dubai ni kutafsiri kwa vitendo namna nchi zinavyotumia mbinu mbalimbali za ubunifu, ugunduzi na ushirikiano katika kuleta maendeleo dunani. Lengo hili linatafsiriwa kwa Kauli Mbiu kuu ya Maonesho hayo ambayo ni “Connecting Minds, Creating the Future’’ ikilenga kubainisha mbinu mbalimbali za ubunifu na kufungua fursa za kiuchumi zilizopo duniani na kuzitumia ipasavyo kwa maendeleo endelevu. Nchi mbalimbali duniani zitajikita katika kuonesha
mafanikio waliyofikia katika kutafsiri kauli mbiu hiyo ikilenga kuonesha Ubunifu, Fur-sa na Mipango endelevu ’Innovation, Opportunity and Sustainability’’.
Tanzania pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji, utalii, viwanda na biashara itajikita katika kauli mbiu ya Mobility ili kuonesha tulipotoka, hatua za mafanikio tulipofikia
pamoja na juhudi za Serikali za kuwekeza katika uanzishwaji na uendelezaji wa Miradi mikubwa ya Kimkakati na tunapoelekea na kupata masoko yatakayopelekea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Pia, katika Maonesho haya kutakuwa na:-;
1. Siku Maalumu ya Tanzania (Tanzania National Day) Siku hii itatumika kuelezea fursa za Kiuchumi, Utalii, Uwekezaji Sanaa na Utamaduni wa nchi kwa washiriki
wote wa Expo na Dunia kwa ujumla. Maadhimisho ya siku hii yatahudhuriwa na Viongozi wa Ngazi za Juu wa Serikali ya Tanzania na Falme za Kiarabu.
2. Kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii- Hii ni maalumu kwa ajili ya kunadi vivutio na fursa za Biashara, Utalii na Uwekezaji nchini ambapo viongozi wa Ngazi
za Juu Serikalini na Wafanyabishara mbalimbali watashiriki ili kweza kukutana na wawekezaji kutoka mataifa mengine duniani.
Aidha, kutakuwa na programu mbalimbali kama vile mikutano ya kibiashara na ziara za mafunzo na Maonesho kwa makundi mbalimbali ya vijana, wanafunzi, wasanii,
wanawake, wabunifu na wavumbuzi wa kisayansi au maarifa asilia ili kuongeza wigo wa Watanzania kushiriki maonesho ya Dunia ya EXPO 2020 Dubai. Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kupitia barua pepe [email protected] ; au kwa simu namba 0800110134 bure bila gharama zozote au kwa simu namba 0714
077646.