Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi vifaa vya kufundishia ambavyo ni GREDA na KOPYRTA kwa chuo cha ujenzi morogoro (MWTI) Katikati ni Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Japhet Y. Maselle na kulia ni Mkuu wa chuo hiko Mhandisi Melkizedeck L. Mlyapatali,hafla iliyofanyika katika chuo hicho Mkoani Morogoro
Vifaa vya kufundishia vilivyo kabidhiwa kwa chuo cha ujenzi morogoro (MWTI) ambapo kulia ni KOPYRTA na kushoto ni GREDA.
……………………………………………………………………………………………………………
NA FARIDA SAIDY, MOROGORO
Wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano ipo katika hatua za mwisho kuanzisha tasisi ya teknolojia ya ujenzi (Institute Of Construction Technology) kwa kuunganisha Chuo cha ujenzi Morogoro na Chuo cha teknolojia stahiki ya Nguvukazi-Mbeya kwa lengo la kuboresha mafunzo yanayotolewa katika vyuo hivyo.
Amesema teknolojia hiyo itasaidia kuzalisha wataalam wa fani mbalimbali za ufundi stadi wenye ujuzi wa kufanya kazi kwa vitendo,ambapo taasisi itakayoanzishwa itatoa mafunzo ya usanifu wa majengo,ujenzi na matengenezo ya barabara,majengo,magari,umeme na mitambo.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu mkuu wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga wakati anakabidhi vifaa vya mavunzo katika chuo cha ujenzi Mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu huyo Amekabidhi Greda moja na Kompyuta 20,ambapo amemuagiza mkuu wa chuo hicho Bwana Melkizedeck Lwiyiso kusimamia matumizi ya vifaa hivyo na kusisitiza kuwa visitumike tofauti na matumizi yaliyokusudiwa na serikali.
Amesema serikali imetoa vifaa hivyo kwa ajili ya wanafunzi,hivyo asitokee mtu amepata dili lake akatumia vifaa hivyo.
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha ujenzi morogoro Bwana Melkizedeck Lwiyiso ameishukuru serikali kwa kuwapatia vifaa hivyo vitakavyowasaidia wanafunzi kusoma kwa vitendo.