Na Mwandishi wetu, Arumeru
MTIA nia John Lang’idare Tanaki Laiser ni miongoni mwa wanachama wa CCM wa Jimbo la Arumeru Magharibi Mkoani Arusha, waliochukua fomu na kurejesha ili kuomba ridhaa ya kugombea nafasi hiyo.
Tanaki akizungumza baada ya kuchukua fomu na kurejesha kwa Katibu wa CCM Wilaya hiyo Camilla Kigosi amesema lengo lake ni kuitumikia jamii ipasavyo katika eneo hilo.
Ameeleza kwamba watu wa eneo hilo wategemee uongozi uliotukuka, unaoheshimu na kuthamini watu na utu wao.
“Uongozi utakaojikita kwenye maendeleo ya watu na vitu, changamoto za Arumeru Magharibi nazijua na nimeziishi, muda utakapowadia tutasema na kutenda,” ameeleza Tanaki.
TAARIFA BINAFSI
Jina kamili – John Lang’idare Tanaki Laiser. Mama anaitwa Esther Shaushi Mollel.
Tarehe ya Kuzaliwa – 10.05.1977
Mahali alipozaliwa – Kijiji cha Ilkiurei, Kata ya Ilkiranyi, Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha.
Kabila – Mmasai/Mwarusha
Dini – Mkristo Mlutheri
Ndoa – Nimeoa na nina Watoto wanne (4)
Mahali anapoishi kwa sasa – Kitongoji cha Namayana, Kata ya Kiranyi Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha
Namba ya simu – +255 752 776 188
TAARIFA ZA ELIMU
Mwaka 1987 – 1993 – Shule ya Msingi Levolosi, Kata ya Levolosi, Wilaya ya Arusha, Mkoa wa Arusha (Darasa la I – VII)
Mwaka 1994 – 1997 – Shule ya Sekondari Ekenywa, Kata ya Kiranyi, Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha (Kidato cha I – IV)
Mwaka 1998 – 2000 – Shule ya Sekondari ya Wazazi Meta High School, Kata ya Mabatini, Wilaya ya Mbeya Mjini, Mkoa wa Mbeya (Kidato cha IV – VI).
Mwaka 2001 – 2004 – Chuo Kikuu Mzumbe , Kata ya Mzumbe, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro (Shahada ya kwanza ya Utawala na Uongozi)
Mwaka 2009 – 2010 – University of Applied Sciences Neu-Ulm, Germany (Stashahada ya juu katika Utawala na Uongozi/ Uongozi wa Afya/Hospitali)
Mwaka 2011 – 2012 – University of Heidelberg, Germany (Shahada ya pili (Shahada ya Uzamili) katika Afya ya Jamii i.e Public Health/International Health)
Mwaka 2019 – 2021 – St. Augustine University – Arusha Campus (Stashahada ya Sheria)
TAARIFA ZA AJIRA/KAZI
Mwaka 2005 – 2006 – Katibu wa Afya/Afisa Rasilimali Watu wa Hospitali ya Endulen – Ngorongoro, Arusha. Hospitali hii inamilikiwa na Jimbo Kuu Katoliki Arusha.
Mwaka 2006 – 2012 – Katibu wa Afya/Afisa Rasilimali Watu wa Hospitali ya Selian Lutheran – Ngaramtoni, Arusha. Hospitali hii inamilikiwa na Kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Kati. Kwa sasa Hospitali hii ina hadhi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha.
Mwaka 2012 – 2019 – Katibu wa Idara ya Afya ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini kati (Promotion). Kusimamia huduma zote za Afya zinazotolewa na Kanisa La Kiinjili La Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Kati – Arusha.
Mwaka 2020 – April 2024 – Katibu Mkuu (CEO) wa Kanisa La Kiinjili La Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, Arusha.
Kwa nafasi ya Katibu Mkuu nilikuwa Msemaji wa Dayosisi, mdhamini wa mali za Dayosisi (The Registered Trustee), kusimamia watumishi wote wa Dayosisi na kuwaongoza Waumini wa Dayosisi walio zaidi ya 600,000.
“Kwa nafasi hiyo pia nilikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Dayosisi na Mkutano Mkuu wa Dayosisi na nilikuwa muandaaji wa vikao hivyo. Pia kwa nafasi yangu ya Katibu Mkuu, nilikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Kanisa zima la KKKT, lakini pia nilikuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Kanisa zima KKKT. Pia nimekuwa mjumbe wa Kamati mbalimbali za Kanisa ikiwepo ile ya kutengeneza Katiba moja ya KKKT.
Mwaka 2024 May hadi leo – Mimi ni Msaidizi wa Katibu wa Idara ya Afya wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Arusha. Ofisi zetu ziko Hospitali ya Selian Lutheran – Ngaramtoni.Majukumu yangu ni kusimamia Hospital tatu (3), Kituo cha Afya kimoja (1), Zahanati sita (6) na Chuo Kimoja cha Uuguzi (Nursing School) kmoja (1). Pia nasimamia Miradi miwili ya Afya ambayo ni Mradi wa Kuthibiti na Kupambana na Virusi vya Ukimwi, Mradi wa Hospice and Pallietive Care (Tiba Shufaa)
KOZI FUPI (CAPACITY BUILDING)
Certificate in Directorship – CiDir
Communication and principles of Protocol – Chuo Cha Diplomasia
Proficiency Human Resources Management Course – TPSC
Resource Mobilization, Strategic thinking and Financial Management
Hospital Management
Tanzania Labor Laws
IPC – IS and Quality Improvement
Good Governance
Community Leadership
MEMBERSHIP AND SKILLS
MEMBERSHIP (UJUMBE KATIKA BODI NA KAMATI
SKILLS (UJUZI)
Arusha District Council Board Member
Protocal and Etiquatte Facilitator
Selian Lutheran Hospital Board Member
Strategic Management Facilitator
Simanjaro District Council Board Member
Project Management
Registered Trustee of ELCT North Central Diocese
Strategic Planning
Member of Executive Council of ELCT
Institutional Policy and Constitution making
Member of General Assembly of ELCT
Leadership and Management
Member of Executive Council of ELCT North Central Diocese
Risk Management
Member of General Assembly of ELCT North Central Diocese
Finance and Planning Management.
UZOEFU KWENYE UONGOZI
“Nikiwa shule ya Msingi nilikuwa Monitor wa Darasa na baadaye nilikuwa Kaka Mkuu wa Shule ya Msingi Levolosi – Arusha,” amesema Tanaki..
“Nikiwa Shule ya Sekondari Ekenywa – O-Level (Arusha), nilikuwa “Head Prefect” Wakati huo huo nilikuwa Mwenyekiti wa UKWATA tawi la Ekenywa, Katibu wa UKWATA Mkoa wa Arusha na vilele vile nilikuwa Katibu Msaidizi wa UKWATA Taifa. UKWATA ni kifupi cha Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania,” amesema Tanaki.
*Nikiwa Shule ya Sekondari Meta High School – A-Level (Mbeya), Nilikuwa “Prefect” wa Shule, Pia, nilikuwa Mwenyekiti wa UKWATA tawi la Meta High School, pia nikawa Makamu Mwenyekiti wa UKWATA Mkoa wa Mbeya na Baadaye nikawa “RAIS” wa UKWATA Taifa,” amesema Tanaki.
Akiwa Chuo Kikuu cha Mzumbe – Morogoro ambacho hapo awali kiliitwa IDM- Mzumbe, alikuwa kiongozi na mmoja wa waanzilishi wa University Student Christian Fellowship (USCF) na baadaye alikuwa Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Mzumbe (MUSO) i.e Mzumbe University Student Organisation.
“Ni wakati huu nikiwa Chuo Kikuu mzumbe, mimi nikishirikiana na rafiki yangu Elibariki Emmanuel Kingu ambaye kwa sasa ni Mhe. Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, tuliweza kuwashawishi wanafunzi wengi kufungua tawi la CCM pale karibu na Chuo – Changarawe na tulimualika Mhe. John Samwel Malechela kuja kutukabidhi kadi za Chama na zile za UVCCM naye akafanya hivyo,” ameeleza.
“Hata nilipokuwa Chuo Kikuu cha Heidelberg nilipokuwa nikisoma Shahada yangu ya pili (Shahada ya Uzamili), nilikuwa kiongozi wa wanafunzi,” ameeleza.
Pia akiwa msharika wa kawaida katika Usharika wake wa Salei na sasa Usharika Tarajali wa Mianzini, amekuwa Mzee wa Kanisa kwa takriban miaka nane.
“Wasifu huu wa John Langidare Tanaki Laiser unaonesha dhahiri shahiri kuwa Bw. Tanaki amezaliwa Kiongozi (Born a Leader) na wakati huo huo akatengenezwa kuwa Kiongozi (Made a Leader) kwa kuhudhuria mafunzo ya Uongozi”.