Na Emmanuel J. Shilatu
1. Tanzania Leo hii ni nchi ya 7 kwa uwekezaji Afrika.
2. Tanzania ya Leo imepanda kwa nafasi 13 katika Mwaka 2016 na Mwaka 2017 na pia ikishika nafasi ya pili kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.
3. Tanzania ya Leo uchumi umekuwa hadi kufikia asilimia 7.2 toka asilimia 5.1 ya hapo awali.
4. Tanzania ya Leo Elimu kuanzia ya Msingi hadi ya Sekondari ni bure. Hapa adui ujinga anapigwa Vita kwa vitendo.
5. Tanzania ya Leo ina miliki ndege zake takribani 8 na hivyo kuifungua Tanzania kiutalii Duniani, kuongeza mapato na kuleta ufanisi na ubora wa usafiri wa anga nchini.
6. Tanzania ya Leo kuanza kutumia usafiri wa treni wa kisasa unaotumia umeme toka ule wa kikoloni uliokuwa unatumia dizeli. Hii itasaidia Watu na mizigo kusafiri kwa haraka, kwa unafuu na hivyo itasaidia ukuaji wa uchumi kwa Kasi.
7. Tanzania ya Leo kesi Mpya zaidi ya 41 za makosa ya ufisadi na uhujumu uchumi zimefunguliwa; Kesi Mpya za rushwa zipatazo 495 zilifunguliwa na Kati ya hizo asilimia 60.14 walifungwa. Pia jumla ya Tsh. Bilioni 127.9 kuokolewa kutokana na matendo ya rushwa.
8. Tanzania ya Leo nidhamu na uwajibikaji kwa Watumishi wa umma imeimarika sana; Uonevu dhidi ya Mtanzania mnyonge umepungua.
9. Tanzania ya Leo Kuna upatikanaji wa dawa za kutosha mpaka ngazi za Vijiji; Vifaa tiba na upasuaji wa kibingwa unafanyika nchini. Suala la Wagonjwa kupelekwa nje ya nchi kutibiwa limepungua Sana.
10. Tanzania ya Leo inanufaika na rasilimali madini yake kwani Sasa nchi inapata gawio sawia la faida za madini (50/50) huku Serikali ikimiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji madini.