Naibu waziri wizara ya afya Mwendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dokta Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi alipotembelea kituo Cha Afya Momela kilichofanyika Halmashauri ya Meru pembeni yake Ni mfadhili wa kituo hicho ambaye pia ni Rais wa shirika la Afrika Amini Alama , Christine Wallner.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kumsikiliza Naibu waziri katika mkutano uliofanyika katika kituo Cha afya Momela kilichofanyika Halmashauri ya Meru(Happy Lazaro)
……………………………………………………………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Serikali imetoa siku 7 kurejeshwa kwa mashine katika kituo Cha afya Cha Momela ili wananchi waweze kuendelea kupata huduma .
Hayo yalisemwa Jana na Naibu waziri wizara ya afya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt.Faustine Ndugulile alipotembelea Kituo cha afya Momela kilichopo Halmashauri ya Meru ,Wilayani Arumeru kufuatia mgogoro uliopelekea kuondolewa kwa baadhi ya huduma na Wafadhili wa kituo hicho Shirika la Africa Amini Alama kuondoa baadhi ya mashine.
Aidha Dokta Ndugulile ameliagiza shirika hilo kurejesha mashine zote zilizokuwa zikitumika katika kituo hicho ndani ya siku 7 ili wananchi waendelee kupata huduma zote zilizokuwa zinatolewa hapo awali.
Alizungumza hayo kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Olkung’wado Kata ya Ngarenanyuki ,ikiwa ni baada ya kikao kati ya uongozi wa Wilaya ya Arumeru,Uongozi wa Halmashauri na wafadhili wa Shirika la Africa Amini Alama ambapo alieleza kuwa serikali yaTanzania ipo tayari kufanya ushirikiano na wadau wa afya kwa kuzingatia Sheria,kanuni ,taratibu na miongozo ya sekta hiyo.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kilipo kituo hicho Dkt. Maneno Focus, Kituo cha afya Momela kimesajiliwa ni mali ya umma na kina watumishi wa Serikali na hupokea dawa toka Bohari ya dawa pamoja na fedha za wahisani mbalimbali zikiwemo fedha za Busket fund.
Aidha, taarifa imeonyesha mwaka 2009 kijiji cha Olkung’wado kilitenga ekari 10 za ardhi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati iliyokamilika 2010 na kukabidhiwa Serikalini ambapo ilisajiliwa mwaka 2012 kama zahanati ya kijiji cha Okungwado momela na mwaka 2013 Serikali iliingia makubaliano ya uboreshaji Zahanati hiyo na wafadhili wa Africa Amini Alama. Mnamo mwaka 2015 Zahanati hiyo ilipandishwa hadhi kuwa kituo cha afya.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Ndg.Emmanuel Mkongo katika kikao alisema Halmashauri hiyo ilishindwa kuridhia ombi la wafadhilli la kubadilisha Kituo cha afya Momela ambacho ni cha Umma kuwa Hospitali ya binafsi ya wahisani (Charitable private Hospital) kwakuwa ni kinyume cha Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo za uendeshaji wa Vituo vya kutolea huduma.
Mkongo alisema Halmashauri inadhamini mchango wa wafadhili wa Africa Amini Alama na ilitaka kumaliza changamoto zilizojitokeza kwa kushirikisha Mamlaka mbalimbali za Serikali kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo za uendeshaji wa Vituo vya kutolea huduma. uendeshaji vituo vya kutolea huduma za afya.
Ndugulile baada ya kikao ametoa mwelekeo wa Serikali kuwa, kituo hicho kitabaki kuwa mali ya umma na kitakapokidhi vigezo kitapandishwa hadhi kuwa Hospitali ya umma na siyo ya binafsi kama wafadhili walivyoomba, ”hatuwezi kutoa kituo cha umma kwa mtu binafsi”amesisitiza Ndugulile.
Kwa upande wa Wafadhili Christine Wallner ambaye ni Rais wa Shirika la Afrika Amini Alama ameishukuru serikali kwa kutatua mgogoro huo na kueleza kuwa shirika lipo tayari kuendelea kufadhili kituo hicho sambamba na kutekeleza agizo la kurejesha mashine maeneo husika,ambapo ameiomba Serikali kuharakisha maandalizi ya makubaliano ya kuboresha utoaji huduma Kituoni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amemuomba Naibu waziri kupokea ombi la Wananchi la kukipandisha hadhi kituo hicho cha afya kuwa Hospitali ili kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za afya, ambapo ametoa wito kwa wananchi kutokuwa sehemu ya kuchochea migogoro .
Mbunge wa Jimbo la Arumeru mashariki, Dkt.John D. Pallangyo ameishukuru Serikali namna inavyowathamini wananchi wake kwa kufanyia kazi ombi lao alilowasilisha la kuomba utatuzi huduma kusitishwa katika kituo hicho cha afya.
Nao Wananchi wa Kijiji cha Olkung’wado Kata ya Ngarenanyuki wameiomba Serikali kuharakisha mpango wa kuandaa makubaliano ya uendeshaji wa kituo hicho pamoja na kukipandisha hadhi kuwa Hospitali