Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisema jambo kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo kwa wataalam (hawapo pichani) katika kikao alichofanya nao mara baada ya ukaguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kulia) akikagua nyaraka ya dawa iliyoandikwa kwa karatasi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ambapo amepiga marufuku na kuwataka kujaza maombi ya dawa kupitia fomu maalum.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiakikagua nyaraka ambayo imeandikwa kwa usahihi kwenye fomu maalum ya maombi ya dawa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi).
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Kilimanjaro (Mawenzi) Dkt. Jummane Karia akisema jambo wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na wataalam katika Hospitali hiyo
………………………………………………………………………………………….
Na Englibert Kayombo, WAMJW – Moshi, Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amepiga marufuku kwa watumishi wa afya katika vituo vya kutolea huduma za afya kutumia karatasi kama njia ya kuidhinisha maombi ya dawa.
Dkt. Ndugulile ametoa marufuku hiyo maara baada ya kubaini mianya ya upotevu wa dawa za Serikali katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini alipokuwa ziarani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi)
“Ni marufuku kuanzia sasa kutumia karatasi za daftari kuomba dawa kutoka idara moja kwenda nyingine, tuandae fomu maalum za maombi” Amesema Dkt. Ndugulile
Ameagiza kuwa dawa zote zinazopatikana katika vituo vya kutolea huduma ziwekwe kwenye fomu za maombi (reiquizitaion form) huku zikionyesha jina la aliyeomba pamoja na kusaini kuthibitisha maombi yake ya dawa.
Amesepa pia mtu au idara ya famasi inayopoke maombi hsyo anatakiwa kuhakikisha maombi hayo na kusaini fomu hiyo.
“Ni marufuku kwa mtu wa famasi kujiongezea dawa kwa maneno ya mdomo au kuambiana, na atakayepokea dawa hizo pia anatakiwa aandike jina lake na kusaini.
Hatua hiyo inakuja mara baada kubaini mianya ya upotevu wa dawa za Serikali ambapo Dkt. Ndugulile amesema “Serikali imewekeza nguvu kubwa sana katika upande wa dawa, lakini pia nyie wataalam ambao mnasimamia mnatakiwa kuhakikisha mnaweka kumbukumbu zenu sahihi ili kudhibiti mianya ya upotevu wa dawa”
“Hapa nnapata mashaka kuwa kuna uptevu wa dawa za Serikali tujirekebishe na kuhakikisha tunatunza vzuri kumbukumbu zetu” Amesema Dk. Ndugulile na kuwataka kuhakikisha wanaweka mifumo ya TEHAMA katika kusimamia maombi ya dawa.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi) Dkt. Jumanne Karia amesema wamepokea maelekezo hayo na kuahidi kuyatekeleza mara moja.
“Tunashuruku kwa maelekezo yako, tutaendelea kuunga mkono Wizara ya Afya na tutatekeleza maelekezo uliyoagiza” Amesema Dkt. Karia.