Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanya mkutano maalum ambapo pamoja na mambo mengine itapokea na kupitia taarifa ya Tathimini ya Kipindi cha Kati (Mid-Term Review) ya Utekelezaji Mpango Mkakati wa hospitali hiyo wa mwaka 2022-2027.
Akifunguo mkutano huo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya MNH, Dkt. Ellen Mkondya ametumia nafasi hiyo kumkaribisha rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Delilah Kimambo na kumtakia kila la heri katika nafasi hiyo yenye majukumu makubwa na kuongeza kuwa Bodi yake itampa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha Dkt. Kimambo anatimiza majukumu yake kikamilifu.
Naye Dkt. Kimambo amemshukuru tena Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kushika wadhifa huo ambapo ameahidi kwa kushirikiana na Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa Hospitali hiyo kutekeleza jukumu hilo kwa weledi ili kuboresha huduma bora kwa wananchi na kuifanya MNH kuwa kitovu cha umahiri cha utoaji huduma za kibingwa na ubingwa bobezi barani Afrika.
Mkutano huo pia umehudhuriwa na Menejimenti ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ambao ndiyo watekelezaji wakuu majukumu ya kila siku ya hospitali hiyo